WANAOZAA NA KUTUPA WATOTO WAWE NA HURUMA: MAITI YA MTOTO WA MIEZI TISA YAOKOTWA IKIWA IMETUPWA VICHAKANI WILAYANI KAHAMA...!!
Maiti ya mtoto huyo |
Mtoto
wa kiume anayekadiriwa kuwa na zaidi ya miezi 9 ambaye hajatambulika
jina lake wala makazi amekutwa ametupwa huku akiwa amefariki dunia
katika kijiji cha Mhongolo Mashariki wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Akizungumzia tukio hilo, Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Aly Manyama amesema kuwa alipigiwa
simu leo majira ya saa 12 na nusu jioni na katibu wa Mwenyekiti wa
kitongoji Chrismas Maganga na kuelezwa juu ya tukio hilo.
Manyama
amesema baada ya kufika eneo la tukio alikuta mwili wa mtoto huyo ukiwa
umeviringishwa katika kitenge na kutupwa kichakani katika eneo hilo.
Hadi
sasa haijafahamika chanzo cha kifo wala wahusika wa kichanga hicho
ambacho kinaonekana kama kimeunguzwa na moto, na Mwili wa marehemu
umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya kahama.
Maiti ya
mtoto huyo ikiwa imewekwa katika kitanda cha kubebea maiti ili kuwekwa katika gari la polisi
Askari Polisi baada ya kupakiza mwili huo |
Wananchi na waandishi wa habari wakiangalia Maiti ya mtoto huyo |
Maiti ya mtoto huyo imetupwa karibu na nyumba hii inayojengwa hapa |
0 comments: