WANAWAKE ZAIDI YA 60 WATEKWA NYARA NIGERIA
Wapiganaji wa Boko Haram wanataka kutawala eneo la Kaskazini mwa Nigera kwa kutumia sheria ya kiisilamu
Inaripotiwa
kuwa wanawake pamoja na wasichana sitini walitekwa nyara Kaskazini
Mashariki mwa Nigeria wiki iliyopita.Ripoti zilizotolewa mwishooni mwa
wiki iliyopita zilisema kuwa ishirini kati yao walichukuliwa na kundi
linaloaminika kuwa Boko Haram.Wanawake hao walitekwa wakati wa uvamizi
uliofanywa katika vijiji vilivyo katika wilaya ya Damboa katika jimbo la
Borno.Wanawake hao inaarifiwa walitekwa nyara katika eneo la vijijini
ambakop mawasiliano ni magumu sana , sababu ya kupata habari hizi
kuchelewa.
Watu wanaotoroka vijiji ambavyo vilishambuliwa, wanasema kuwa wanawake na wasichana sitini walitekwa nyara wiki jana.
Baadhi ya
watoto waliotekwa ni wadogo sana wa umri. Moja ya vijiji
vilivyoshambuliwa ni kile cha Kummabza kilicho katika eneo la Damboa
katika jimbo la Borno.
BBC hata
hivyo haijaweza kuthibitisha idadi kamili ya watu waliotekwa nyara. Hali
hii imefanywa kuwa ngumu'kwani maafisa wa eneo hilo bado hawajatoa
tamko lolote kuhusu kisa hiki labda kutokana na hofu juu ya maisha yao.
Sio jambo
la kushangaza kwamba tangu kutekwa nyara kwa wasichana miambili wa
shule kutoka Chibok , wanawake wengine wametekwa nyara
Vijiji vingi
katika eneo la Kaskazini mwa Nigeria, vinakumbwa na utovu wa usalama na
wakati ambapo Boko Haram wanapofanya shambulizi,wao huchukua muda mrefu
wakifanya uporaji na mauaji.
Mwishoni mwa wiki, idadi kubwa ya watu waliuawa karibu na eneo la Chibok.
Zaidi ya wasichana 200 wa shule walitekwa nyara eneo la Chibok mwezi Aprili.
Walitekwa nyara kutoka shule yao ya mabweni na wapiganaji wa Boko Haram.
Serikali ya Nigeria imekuwa chini ya shinikizo kali za kuitaka ifanye jitihada za kuwaokoa wasichana hao
0 comments: