WANANCHI WAANDAMANA KUPINGA KOMBE LA DUNIA BRAZIL
Maelfu ya wenyeji wasio na makao mjini Sao Paolo waliandamana nje ya uwanja utakaoandaa mechi ya kwanza ya kombe la dunia alhamisi ijayo wakipinga gharama ya juu ya mashindano hayo.
Maandamano
hayo yaliwadia siku moja tu baada ya rais wa Brazil Dilma Rousseff
kuwahakikishia wageni na mashabiki wa kandanda kuwa kamwe hatoruhusu
maandamano yatie doa kwenye kipute hicho cha kombe la dunia.akriban
waandamanaji 10,000 waliziba barabara zote mjini Sao Paolo
wakiishinikiza serikali ya bi Rousseff iwekeze katika sekta ya afya
elimu na ipunguze gharama ya juu ya usafiri wa umma.
Zaidi
ya watu milioni moja waliandamana katika barabara za miji yote ya
Brazil wakishinikiza serikali kupunguza ubadhirifu wa fedha na kupunguza
matumizi yake kwa maandalizi ya kombe la dunia na yale ya Olimpiki
yatakayofanyika mjini Rio mwaka wa 2016.
Licha
ya hakikisho la rais Rousseff wafanyikazi wa reli walitishia kuanza
mgomo upya huku polisi wa trafiki mjini Sao Paolo pia wakitishia kuanza
mgomo Alhamisi.
Mapema
wiki hii serikali iliwaongezea polisi wote mshahara ilikuzuia mgomo
uliotishia kuporomosha hali ya utengamano huku fainali ya kombe la dunia
likinukia.
Serikali imeahidi kutumia polisi na hata jeshi la taifa kudumisha amani na utengamano wakati wa kombe la dunia.
0 comments: