WAFUKUA MAKABURI NA KUIBA VIUNGO VYA MAITI NA KWENDA KUVIUZA
Viongozi
wa mashitaka nchini Brazil , wanachunguza madai kuwa viungo vya miili
vinatolewa kwa miili ya watu wasiojulikana na kuuzwa kwa ajili ya
utafiti wa kimatibabu.Viongozi wa mashitaka wameambia BBC
kuwa viungo vinataolewa kwa miili ya watu waliofariki bila ya kufanyika
juhudi za kuwatafuta jamaa zao watu hao ili kupata ruhusua kutoka
kwao.Hadi hivi karibuni, maiti zilizopatikana kando ya barabara au
katika hospitali za umma huzikwa katika makaburi ya umma ikiwa hakuna
aliyekuja kudai miili hiyo kwa muda wa masaa 72.
Hata
hivyo moja ya shirika linalodaiwa kufanya uhalifu huo wa kuuza viungo
vya miili ya watu wasiojulikana limekanusha madai hayo.
Kuuza viungo vya miili ya watu ni kinyume na sheria ya Brazil.
Uchunguzi
huu ulioanza mjini Sao Paulo, mwaka jana, ulianzishwa na polisi
kutokana na madai ya familia kwamba maafisa wakuu hawakuwashauri kabla
ya kuzika jamaa zao waliofariki katika makaburi ya umma ya Perus.
Baadaye
mmoja wa walioshuhudia vitendo hivyo walifahamisha polisi kuwa viungo
hutolewa kwa miili ya wafu na kutumiwa kwa utafiti wa kimatibabu bila
idhini ya jamaa wa wafu.
Hata hivyo viongozi wa mashitaka wanasema kuwa hawana ushahidi wa kutosha kuthibitisha madai ya biashara ya viungo vya binadamu.
Lakini
uchunguzi wa polisi ulibaini kuwa katika miaka 15 iliyopita, miili 3000
ilitolewa katika vyumba vya kuhifadhia maiti na kuzikwa katika makaburi
ya umma , licha ya kwamba zilikuwa na stakabadhi za kuzitambulisha.
Shirika
la SVO linaloendeshwa na walimu kutoka katika chuo kikuu cha Sao Paulo,
linasema kuwa kwa kawaida wao hutumia miili tu ambayo imeshatambulishwa
wanapotafuta viungo vya utafiti.
Walimu hao wanasema huwa hawatumii miili ambayo wenyewe hawajulikani.
>.>>BBC
0 comments: