Add caption
TIMU
ya Mpira wa miguu ya Mbeya City Fc inayomilikiwa na Halmashauri ya Jiji
la Mbeya imeanza kujihakikishia kufanya vizuri zaidi kwa msimu ujao
baada ya kupata rasmi mdhamini.
Kampuni
ya Bin Slum Company Limited yenye makao makuu jijini Dar Es Salaam
ndiye kampuni ya kwanza kukubali kuwa mdhamini wa timu hiyo kwa miaka
miwili kwa kitita cha shilingi Milioni 360.
Utilianaji
sahihi wa mkataba umefanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi za Halmashauri
ya Jiji la Mbeya baina ya Uongozi wa Kampuni hiyo na Halmashauri ya
Jiji la Mbeya mbele ya vyombo mbali mbali vya habari.
Akizungumza
na vyombo vya habari katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa kampuni hiyo,
Mohamed Binslum, alisema kampuni yake imefikia makubaliano hayobaada ya
kuridhika na uongozi wa Mbeya city namna ulivyojipanga katika kuendesha
timu.
Binslum
alisema pia kampuni yake imeridhika namna timu hiyo ilivyopata mwitikio
mkubwa kutoka kwa wananchi wa Jiji la Mbeya pamoja na mikoa ya Nyanda
za juu kusini.
Aliongeza
kuwa katika mkataba huo wenye thamani ya Shilingi Milioni 360 kampuni
hiyo itakuwa ikitangaza bidhaa zake ambazo ni RB Battery katika Jezi za
Timu ya Mbeya city na nyuma ya jezi chini ya namba itaandikwa jina la
kampuni la Binslum Tyre Company.
Mkurugenzi
huyo alisema kuingia Mkataba na Mbeya city ni fursa pekee ya Kampuni
kutangaza bidhaa zake za Betri aina ya RB ambazo zina soko kubwa Mkoani
Mbeya pamoja na bidhaa zingine ambazo ni matairi aina ya Double star na
vee rubber.
Kwa
upande wake Katibu wa Timu ya Mbeya city, Emmanuel Kimbe, mbali na
kuishukuru kampuni hiyo kwa kukubali kuwa mdhamini wa Mbeya city pia
alimuahidi kutekeleza kile mdhamini anachotarajiwa kukipata kwenye timu
hiyo.
Alisema
Mbeya city inadhumuni la kutangaza bidhaa za Bin Slum kupitia jezi za
mechi za ndani, Nje na mazeozi ikiwa ni pamoja na timu kuendelea
kufanya vizuri.
Aliongeza
kuwa mbali na kupata mdhamini lakini wamiliki wa timu pia wataendelea
kufanya majukumu yao kwa ajili ya timu kama kawaida na kuongeza kuwa
mkataba huo unaanza Juni Mosi Mwaka huu hadi Mei 31, 2016.
Naye
kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Dk. Samwel
Lazaro,alisema Halmashauri imepata faraja kubwa kupata mdhamini kutokana
na Halmashauri kutokuwa na fedha za kutosha kuweza kuendesha timu.
Alisema
kuendesha timu kunahitaji kuwa na uchumi mkubwa ambao Halmashauri haina
hivyo kupitia mdhamini huyo timu ya Mbeya city itafanya vizuri zaidi
katika msimu ujao.
Mwisho.
|
0 comments: