TAARIFA ZILIZOSAMBAA KUHUSU WAZIRI WA ELIMU SHUKURU KAWAMBWA
TAARIFA TOKA BAGAMOYO
Ndg Watanzania,WanaBagamoyo na wapenda maendeleo, kwa niaba ya
CCM-Bagamoyo na Ofisi ya Mbunge-Jimbo la Bagamoyo napenda kuleta kwenu
Masikitiko yetu kwa niaba ya Chama na Familia ya Mheshimiwa Mbunge
Shukuru Jumanne Kawambwa kutokana na Usumbufu ambao umesababishwa na
habari zinazoenezwa Mitandaoni kwamba Mheshimiwa Kawambwa amekumbwa na
Umauti akiwa njiani anaelekea Mwanza.
UKWELI
Mheshimiwa Shukuru Jumanne Kawambwa yupo Nchini Canada Akitimiza
majukumu yake. Hivyo Watanzania na wana Bagamoyo mnaombwa radhi kwa
usumbufu uliotokea na kwamba Mheshimiwa Mbunge yuko na Afya njema na
utekelezaji wa Majukumu unaendelea kama kawaida.
Ndg.Ridhiwani Kikwete (Mnec)
Mbunge -Chalinze
0 comments: