PICHA ZILIZOKOSA MAADILI ZIKIWEMO CHA KUMCHAFUA MHE CAPTEN JOHN KOMBA NA ZILE ZA AKINA DIAMOND NA WEMA SEPETU ZACHAFUA HALI YA HEWA BUNGENI DODMA.
Katika majibu yake waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia Prof. Makame Mbarawa anasema “Mhe. Spika kuhusu picha zisizokuwa na maadili zinazowekwa katika mitandao na watu maarufu na hata wasiokuwa maarufu serikali imeanza kuandaa kanuni zitakazokuwa zikifuatilia Online Content ambapo itaanza kuchukua hatua baada ya kufuatilia juu ya picha hizo na kuchukua hatua madhubuti”.
Baada ya kauli hiyo Spika wa bunge Mhe. Anne Makinda alikazia akitaka majibu juu ya picha za juzi zilizosambaa zikimuonyesha Mhe. Komba akiwa na binti mdogo ambazo mwenyewe alisema si zake na wabunge kuonekana wakitaka majibu ambapo Mhe. Mbarawa anasema.
“Mhe. Spika kuhusu picha za juzi zilizosambaa mitandaoni tunazifuatilia kujua zimeanzia wapi na taarifa zake zikoje kwani hata mimi bado sijaziona ila tutachukua hatua tutakapobaini zilipotoka.”
0 comments: