MPYA KABISA: NAFASI ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO ZATANGAZWA RASMI LEO HII--16800 WAKOSA SHULE
Nafasi za kujiunga
na kidato cha nne mwaka 2014 kwa wanafunzi waliomaliza mwaka jana
zimetangazwa rasmi muda huu jijini dare s salaam na naibu waziri wa
TAMISEMI Bw KHASIM MAJALIWA ambapo zaidi ya wanafunzi 16800 wamekosa
nafasi hizo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo upungufu wa shule za
kidato cha tano
Akitangaza majina na shule walizopangiwa wanafunzi hao Mh MAJALIWA
amesema kuwa jumla ya wanafunzi 54085 sawa na alimilia 75.61 ya
wanafunzi 71527 waliostahili kuingia kidato cha tano mwaka huu
wamechaguliwa huku wavulanai ni 31352 wakati wasichana ni 22733 ambapo
ni sawa na ongezeko la wanafunzi 20402 kwa kulinganisha na wanafunzi
33683 walochaguliwa mwaka jana.
Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na shule mbalimbali wataanza kuripot
katika meneo yao tarehe 10 julai mwaka huu ambapo mwisho wa kufika
katika shule walizopangiwa ni tarehe 30 julai mwaka huu ambapoamesema
kuwa kwa wale ambao watakuwa hawajiripot hadi tarehe hiyo nafasi zao
zitajazwa na waliokosa nafasi.
0 comments: