MENGINE YA KOMBE LA DUNIA BRAZIL
Kwa
mara ya kwanza katika historia ya Kombe la Dunia, rangi itatumika na
waamuzi kuweka alama uwanjani wakati wa free kick. Rangi hiyo ambayo
hutengenzwa kwa kutumia zaidi maji, itatumika kuweka alama mahala hasa
kosa au 'foul' ilipotokea ili mpira uwekwe hapo bila kusogezwa. Pia
rangi hiyo itatumika kuchora mstari ambao timu inatakiwa "kujenga ukuta".
Hii
itaepusha wachezaji kuusogelea mpira kabla free kick haijapigwa. Rangi
hiyo ni nyeupe na hufutika baada ya kama dakika moja. FIFA iliidhinisha
matumizi ya rangi hiyo katika Kombe la Dunia 2014, baada ya kutumiwa na
kupata mafanikio katika Kombe la Dunia kwa vijana chini ya miaka 20,
mwaka 2013, Kombe la Dunia chini ya miaka 17, mwaka 2013, na katika
Kombe la Dunia la vilabu mwaka 2013.
0 comments: