MASKINI YA MUNGU SOMA HAPA ALICHOANDIKA FROLA MBASHA HII LEO.
Math5:44 Lakini mimi nawaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi.
‘
Mungu wewe ni Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu. wewe ni Mkuu sana, wewe
ni mwanzo tena mwisho zaidi yako hakuna na hatakuwepo. umesema ktk
1wathesalonike5:18 shukuruni kwa kila jambo maana hayo ni mapenzi ya
Mungu kwenu ktk kristo Yesu. ahsante Mungu maana wewe uliijua jana
yangu, leo na kesho itakuwaje.Mungu wa amani unitakase kabisa nafsi
yangu, mwili wangu na roho yangu unihifadhi, wewe BWANA ni mwaminifu.
Ktk Isaya43;19
umesema,Tazama nitatenda neno jipya: sasa litachipuka je hamtalijua
sasa? nitafanya njia hata jangwani na miito ya maji nyikani. BWANA
mapenzi yako yatimizwe, tenda lililo kusudi lako juu yangu. ktk
Math14:14 umesema, mkiniomba neno lolote kwa jina langu nitalifanya.
ukasema ktk Marko10:27 Yesu akawakazia macho akasema, kwa wanadamu
haiwezekani, bali kwa Mungu sivyo: maana yote yanawezekana kwa Mungu.
Maombolezo3:31-32
Kwa kuwa BWANA hatamtupa mtu hata milele, maana ajapo mhuzunisha
atamrehemu kwa kadiri ya wingi wa huruma zake.
Mungu inua moyo wangu sasa,
wewe ndiyo msaada pekee wa kweli. Ninaamini utatenda makuu kama
ilivyoandikwa ktk Zaburi 108;13 Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu,
maana yeye atawakanyaga watesi wetu. Bwana wewe ni mtu wa vita, Bwana
ndilo jina lako,pigana sasa ninakuachia wewe.
ninashuka mbele
zako ninaungana na wenye uhai wanne ktk Ufunuo4;6-11 kukuabudu wewe
nikisema, 11 Umestahili wewe BWANA wetu na MUNGU wetu,kuupokea utukufu
na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa
sababu ya mapenzi yako vilikuwako navyo vikaumbwa.
0 comments: