MARCO REUS APATA MAJERUHI MABAYA UJERUMANI IKISHINDA 6-1 DHIDI YA ARMENIA, HATARINI KUZIKOSA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA
Kiungo wa Ujerumani, Marco Reus akiwa ameshika kifundo chake
cha mguu wa kushoto baada ya kuumia katika mchezo dhidi ya Armenia
Reus akitibiwa na madaktariwa timu ya taifa ya Ujerumani.
Reus akitolewa uwanjani kwa matibabu zaidi.
PIGO!, Marco Reus hatihati kucheza fainali za kombe la dunia
baada ya jana kupata majeruhi ya kifundo cha mguu katika ushindi wa mabao 6-1
ambao Ujerumani ilivuna dhidi ya Armenia ikiwa ni pasha pasha kabla ya kuanza
kombe la dunia wiki ijayo.
Nyota huyo Borussia Dortmund alianguka chini baada ya
kugongana na kiungo wa Armenia, Artur Yedigaryan na kuambulia kuumia na kuzua
hofu kubwa kwa mashabiki wa Ujerumani na benchi zima la ufundi.
Reus aliachwa amelala chini kwa maumivu makali na kupatiwa
matibabu uwanjani kabla ya kutolewa katika mchezo huo kabla ya muda wa
mapumziko.
Nyota huyo mwenye miaka 25 aliripotiwa kushindwa hata kuvaa
kiatu katika mguu wake wa kushoto na imeelezwa kuwa alipelekwa moja kwa moja
hospitali kwa ajili ya uchunguzi wa kina.
Joachim Low anajiandaa kucheza na Ureno juni 16 katika mechi
ya ufunguzi, na inawezekana Reus akazikosa fainali za kombe la dunia mwaka huu
nchini Brazil.
Akizungumza baada ya mechi, Low alisema: "Tuna
matarajio kuwa atapona. Lakini inaonekana kuwa mbaya sana. Tunaweza kumuita
mchezaji mwingine saa 24 kabla ya mchezo wa kwanza".
Bosi wa Ujerumani, Joachim Low (wa tatu kutoka kushoto)
alionekana kuwa na wasiwasi baada ya Reus kutolewa nje ya uwanja.
0 comments: