HEEE! DOKTA AKUTWA AKIJARIBU KUMCHOROPOA MIMBA DENTI,MSAIDIZI WAKE AANGUA KILI
KABAANG! Dokta mmoja aliyefahamika kwa jina la Herman amenaswa katika dispensari moja iliyopo Buguruni Kwamnyamani jijini Dar akijiandaa kumtoa mimba mwanafunzi. |
Denti huyo akilia.
Kaka huyo alitanguliwa katika dispensari hiyo na kubana sehemu
kumsubiri mdogo wake huyo afike ‘kutoa mimba’ huku makamanda wa OFM
wakiwa wameseti mitambo yao maalum katika kila engo ya eneo hilo.Majira ya saa tisa, mwanafunzi huyo alifika hapo akiwa ameongozana na kijana mmoja aliyesetiwa kuwa mpenzi wa mwanafunzi huyo na kuongea jambo (kumpa fedha) na daktari akiingia chumbani akiongozana na mwanafunzi huyo huko akiwa na vifaa maalum vya kutolea mimba. |
Nesi,dokta chini ya ulinzi.
Baada ya kusubiri kwa dakika tano, kaka wa mwanafunzi huyo na
makamanda wa OFM waliingia katika chumba hicho na kumkuta daktari huyo
akiwa katika pilipilika za kumtoa mimba mwanafunzi huyo ambaye alikuwa
amelala chali.OFM ilifanikiwa kunasa meseji mbalimbali za daktari huyo zilizokuwa zikielekeza namna ya kufanikisha zoezi hilo la utoaji mimba. Majirani ambao walishuudia tukio hilo walipongeza sana OFM kwa kumnasa daktari huyo kutokana na kukithiri kwa tabia hiyo dispensarini hapo. ”Jamani mmefanya vizuri sana kuja kukomesha mchezo huu hapa tumelalamika sana lakini hatusikilizwi,” alisema mzee mmoja aliyejitambulisha kwa jina la mzee Hamisi. |
0 comments: