HABARIII MBAYAAA......Rais Jacob Zuma alazwa hospitalini
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amelazwa hospitalini kwa uchunguzi wa kiafya .
Taarifa
hii ni kwa mujibu wa maafisa kutoka kwa ofisi yake. Taarifa hiyo ilisema
kuwa Zuma atalazimika kumpumzika kwa muda ingawa ataendelea na majukumu
yake ya kitaifa akiwa nyumbani.
Bwana
Zuma ambaye alihusika na harakati dhidi ya utawala wa kibaguzi, ana umri
wa miaka 72 na aliapishwa kwa muhula wa pili baada ya uchaguzi mkuu
tarehe 24 mwezi Mei, ambapo chama chake ANC kilishinda uchaguzi
huo.“Hapo jana Ijumaa Rais Zuma alishauriwa kupumzika hasa baada ya
msimu wa uchaguzi kukamilika wiki chache zilizopita.Madaktari
hawajaeleza wasiwasi wowote kuhusu afya yake.’’
Baraza
lake la mawaziri, lina kibarua kigumu kukabiliana na uchumi wa nchi hiyo
unaoendelea kudorora kila kukicha pamoja na ukosefu wa ajira.
Wadadisi wanasema asilimia 25 ya wananchi hawana ajira.
0 comments: