BAADA YA VITISHO VYA MAGAIDI ANGALIA PICHA ULINZI MKALI WA RAISI WA KENYA UHURU KENYATTA ULIVYO SASA


suBaada ya kuchafuka kwa hali ya usalama nchini Kenya kutokana na tishio la magaidi wa Al Shabaab sasa ulinzi unaomlinda raisi wa Kenya umeongezwa maradufu. Kila sehemu anayotembelea ulinzi umeongezwa kuanzia magari, wanajeshi na hadi polisi.

 uhuru3

Mpya imetokea wiki iliyoisha katika uwanja wa Nyayo stadium ambako kulikua na  sherehe za kitaifaambapo kulikua na ulinzi mkali sana kiasi kwamba kila mtu aliyeingia katika uwanja huo alikaguliwa. Ndani ya uwanja alitakiwa kuingia mtu tu bila ya mzigo mwingine wowote hata kama una chupa ya maji hukutakiwa kuingia nayo.


Mbali na ulinzi mkali lakini kitu kilichowaacha midomo wazi watu ni uwepo wa magari mawili mapya katika msafara huo. Gari la kwanza ni alilokua akitumia raisi Kenyata ambalo lilikua limezungukwa na vioo maalum vya kuzuia risasi. Mfano mzuri ni kwa wale waliowahi kuliona gari la kiongozi wa kanisa katoriki lilivyo. Hii ni kwa mara ya  kwanza kwa raisi Kenyata kutumia gari la aina hiyo tangia kawa kiongozi.
 uhuru4
Gari ya pili ni RCV Survivor I gari hii ni gari ya kivita na inaweza kuhimili pilika pilika zote kwani haiingizi risasi na hata ikipigwa bomu hailipuki. Habari Bongoclan ilizozipata kutoka Kenya ni kua matumizi ya gari hiyo nikumhifadhi raisi endapo kutatokea tukio lolote la hatari. Gari hiyo inakuja na silaha aina ya machine gun kwa juu kwa ajili ya kuongeza ulinzi zaidi. Pia gari hili linauwezo wa kutambua mabomu yaliyopo umbali wa hadi kilometa 2.
uhuru6
Kwa ulinzi huu alionaa raisi wa Kenya ni wazi kua yeye ndio raisi mwenye ulinzi mkali kuliko maraisi wote wa Afrika.

0 comments:

Copyright © 2013. MSANGIBIN ALLY - All Rights Reserved
Customized by: MSANGIYUSUPHALY | Powered by: KIINICHAHABARI
Designed by: http://kiinichahabaribongo1.blogspot.com/