VIWANGO VYA WACHEZAJI: ANGEL di MARIA NDIYE NYOTA WA MCHEZO WA FAINALI YA UEFA REAL IKITWAA `NDOO` YA 10, SHUKURANI KWA BAO LA BALE DAKIKA ZA NYONGEZA
Iker Casillas - Alifanya kosa kubwa na kufungwa bao la kwanza baada ya kutoka golini na kushindwa kuzuia mpira wa kichwa uliopigwa na Diego Godin. Alikuwa chini ya kiwango. Anapata alama 5Daniel Carvajal - Alicheza vizuri na kuisaidia timu mara kadhaa. Anapata alama 6Raphael Varane - Alisimama imara kulinda lango lao na alihusika kuwachinja vijana wa Diego Simeone katika dakika za mwisho. Anapata alama 6.
Sergio
Ramos - Alioneshwa kadi ya njano katika kipindi cha kwanza na mara
nyingi alikuwa kama kachanganyikiwa mpaka alipofunga bao la kusawazisha
kwa njia ya kichwa na kuwapeleka dakika za nyongeza. Anapata alama 7.
Fabio Coentrao - Alijituma sana, lakini alitolewa mapema kipindi cha pili. Anapata alama 5.Luka
Modric - Alikuwa na kazi nyingi katika sehemu ya kiungo, lakini
kiukweli alishindwa kuleta madhara kama alivyozoeleka. Anapata alama 6.


Sami Khedira - ilishangaza kumuona katika kikosi cha jana baada ya kukaa nje kwa muda mrefu kutokana na majeruhi ya goti na alitoa mchango wake kabla ya kutolewa. Anapata alama 6.
Angel
Di Maria - Alikuwa bora kwa muda wote wa mchezo na ubora wake ndio
uliobadilisha mchezo na kupata ushindi. Anapata alama 8.
Gareth
Bale - Alionekana kukosa umakini na kupoteza nafasi za kufunga na
kuleta mashaka juu ya gharama kubwa iliyotumika katika usajili, lakini
katika dakika za nyongeza alifunga bao muhimu mno, kama alivyofanya
katika fainali ya Copa del Rey. Ananapa alama 6.
Cristiano
Ronaldo - Alipiga vizuri mpira mmoja wa adhabu uliookolewa na mpira
mmoja wa kichwa ambao haukulenga lango. Hakuwa fiti, japokuwa alifanya
kazi nzuri dakika za mwisho na kuzalisha penati aliyofunga mwenyewe.
Anapata alama 6.
Karim Benzema - Wakati wote wa mchezo hakuwa fiti kabisa. Anapata alama 5
Wachezaji wa akiba walioingia:
Isco - Alijaribu kuongeza nguvu kiasi. Anapata alama 6
Marcelo
- Huyu ndiye aliyebadilisha mchezo kiuhalisia. Aliiongeza makali Real
katika safu ya ushambuliaji na alifunga bao la tatu. Anapata alama 7.

Safi jembe: Pepe na Gareth Bale wakishangilia wakati wa sherehe ya ubingwa baada ya mechi.

Viwango vya wachezaji wa Atletico Madrid:
Thibaut
Courtois - Alikuwa salama muda wote, aliokoa mipira michache na kuokota
kwenye nyavu mpira mmjo wa Sergio Ramos katika dakika za kawaida. Na
aliokota mipira nyavuni mara tatu katika dakika za nyongeza. Anapata
alama 6.
Juanfran
- Ni ngumu kumkosa beki yeyote wa Atletico. Dakika 30 za nyongeza
zilikuwa nyingi sana kwake, lakini alipambana. Anapata alama 6
Miranda - Kwa mara nyingine, alifanya kazi kubwa mno. Anapata alama 6.
Diego
Godin - Aliifungia Atletico bao la kuongoza na bao lake la 6 msimu
huu, ni wiki moja tu ambapo bao lake liliwapa ubingwa wa La Liga.
Alifanya kazi kubwa na atakumbukwa daima. Anapataalama 7
Filipe Luis - Bale alimkimbiza sana, lakini alijitahidi kumzuia. Anapata alama 6
Raul
Garcia - Alioneshwa kadi dakika za mwanzoni baada ya kumfanyia madhambi
Di Maria, lakini hakukata tamaa. Mchezo ulibadilika baada ya kutolewa.
Anapata alama 7


Tiago
- Alikuwa na bahati kwasababu Bale hakuwaadhibu kwa makosa yake katika
kipindi cha kwanza, lakini alifanya jitihada kubwa. Anapata alama 7.
Gabi - Alikuwa bora muda mwingi wa mchezo. Alitoa penati ya haki kabisa. Anapata alama 7.
Koke - Alicheza kwa nidhamu kubwa na kujitolea. Anapata alama 7
Diego Costa - Alianzishwa licha ya kuwa na majeruhi ya nyama za paja, na alicheza dakika 9 tu. Anapata alama 4.
David
Villa - Alikimbiza mara kadhaa na kuwapa shida mabeki wa Real, lakini
Atletico walishindwa kuendeleza kasi yao ya kushambulia na kumfanya
asifanye kazi yake. Anapata alama 6
Wachezaji wa akiba walioingia:
Adrian: Aliingia dakika za mapema kipindi cha kwanza na alitoa mchango mkubwa. Anapata alama 7
Jose Sosa: Hakufanya kazi yake wakati alikuwa anahitajika sana. Lakini alijitahidi. Anapata alama 6.
Toby Alderweireld - Hakuweza kuwazuia Real dakika za nyongeza. Anapata alama 5 .


0 comments: