UKATILI!! BABA AUA MTOTO WAKE WA MIAKA MITATU KWA KIPIGO,KISA NI MKOROFI HAMSIKILIZI BABA YAKE
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita-Joseph Konyo |
Ukatili
dhidi ya watoto umeendelea kutokea katika jamii ambapo mtoto James
Wilson(3)mkazi wa kijiji cha Misri kata ya Bugalama wilayani Geita
mkoabi Geita ameuawa kwa kupigwa baba yake mzazi kwa madai kuwa mtoto
huyo amekuwa hamsikilizi baba yake kwa sababu ya ukorofi.
Akizungumzia tukio hilo diwani wa kata ya
Bugalama Samweli william amesema baba mzazi wa mtoto huyo Wilson Chimba(46) alimtuma mtoto kununua mafuta alipokataa akaanza kumpiga.
Bugalama Samweli william amesema baba mzazi wa mtoto huyo Wilson Chimba(46) alimtuma mtoto kununua mafuta alipokataa akaanza kumpiga.
Kufuatia
kipigo hicho mtoto huyo alikwenda kujificha kwa jirani yake na siku
iliyofuata baba mzazi alipomfuata mtoto huyo kisha kumpiga hadi kumuua.
Jeshi
la polisi mkoani Geita limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba
tayari limemkamata mtuhumiwa huyo kwa kitendo hicho cha kinyama.
0 comments: