POLISI WAMGUNDUA KINARA WA MTANDAO WA WIZI KATIKA MABENKI JIJINI D’SALAAM
Kamishna kova leo alipoamua kuitoa hadharani picha ya mtuhumiwa huyo mbele ya wanahabari ili apatikane mara moja
Jeshi la
Polisi Kanda Maalum D’Salaam limefanikiwa kumbaini mtuhumiwa mhimu
ambaye ni kinara wa mtandao wa wizi katika mabenki ambaye anajulikana
kwa jina la RONALD S/O MOLLEL umri miaka 37, mfanyabishara na mkazi wa
Kimara Bonyokwa Jijini D’salaam.
Mtuhumiwa
huyu amekimbilia mafichoni mara baada ya tukio la ujambazi katika Tawi
la Benki ya Barclays Kinondoni lililotokea tarehe 15/4/2014 ambapo
majambazi walifanikiwa kupora kiasi kikubwa cha fedha
T.Shs.390,220,000/= , USD 55,000/= na EURO 2150/=. Aidha sasa
imefahamika kwamba mtuhumiwa huyu ni mume wa mtuhumiwa wa kwanza katika
tukio la Barclays Benki aitwaye ALUNE D/O KASILILIKA @ ALUNE D/O MOLLEL ,
miaka 28, Mkazi wa Kimara Bonyokwa ambaye ni Meneja wa Benki Tawi la
Barclays Kinondoni. Mtuhumiwa Mollel anatafutwa kwa kila hali kwa vile
yeye ndiye alikuwa kinara wa kupanga tukio hilo la Barclays na mara
baada ya tukio ametoroka na kiasi kikubwa cha fedha hizo zilizoibiwa.
RONALD S/O MOLLEL ambaye ndiye mtuhumiwa wa ujambazi katika mabenk mbalimbali hapa jijini dar es salaam
Zipo
taarifa za kuaminika kuwa mtuhumiwa huyu amekuwa akipanga na kushiriki
kikamilifu katika matukio mbali mbali ya uhalifu mkubwa ikiwa ni pamoja
na kuongoza vikundi vya majambazi vilivyowahi kupora katika mabenki
mbali mbali katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Mtuhumiwa huyo ni
hatari kwani ana mtandao na watumishi muhimu katika matawi mbali mbali
ya mabenki kwa lengo la kufanikisha uhalifu katika mabenki hayo.
Endapo utamona mtu huyu toa ripot mahali popote hata kwa mmiliki wa blog hii
Jeshi la
Polisi limelazimika kutoa picha yake hadharani kwa kutumia dhana ya
ulinzi shirikishi ili mtuhumiwa huyu akionekana akamatwe na taarifa
zitolewe katika kituo chochote cha Polisi ikiwa ni lengo la polisi
kupambana na uhalifu katika dhamira ya kuzuia uhalifu, kulinda maisha na
mali za wananchi.
Zawadi
nono ya fedha taslim itatolewa kwa siri kwa mtu yeyote atakayetoa
taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa mtuhumiwa huyu. Pamoja na maelezo
hayo mtuhumiwa mwenyewe sasa anapewa fulsa ya kujisalimisha katika kituo
chochote cha polisi kabla ya kukamatwa kwa njia nyingine.
0 comments: