PICHA KUTOKA OFISI YA MAKAMU WA RAIS-IKULU:MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHANI MSIBA WA MKE WA KATIBU MKUU WA WIZARA YA FEDHA

Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Adama Malima, akizungumza machache katika shughuli hiyo ya kuhani msiba huo.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha mke wa Katibu Mkuu wa Wizara
ya Fedha na Uchumi, Dkt. Servacius Likwelil, wakati alipofika kumfariji
Katibu huyo nyumbani kwake Boko Jijini Dar es Salaam, jana jioni.
Mazishi yanatarajia kufanyika leo jioni kwenye Makaburi ya Kinondoni.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akijumuika na waombolezaji katika msiba wa mke wa Katibu Mkuu wa Wizara
ya Fedha na Uchumi, Dkt. Servacius Likwelil, wakati alipofika
kumfariji Katibu huyo nyumbani kwake Boko Jijini Dar es Salaam, jana
jioni. Mazishi yanatarajia kufanyika leo jioni kwenye Makaburi ya
Kinondoni.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
0 comments: