IRENE PAUL ATESWA NA BIFU LA KUAMBIANA, "anisamehe huko aliko"
MKALI wa filamu za Bongo, Irene Paul ameweka wazi kuwa anateswa na bifu lake na marehemu Adam Kuambiana kwani amefariki dunia wakiwa wamekorofishana.
Irene alisema alitofautina na
Kuambiana alipokuwa akiigiza Sinema ya Broken Family, miezi kadhaa
iliyopita lakini hadi jamaa huyo anapatwa na umauti, hawakuwa na
maelewano.
“Mimi nilikuwa na hasira, marehemu
pia. Tukapishana kauli na kurushiana maneno makali, nawashauri wasanii
tuache bifu maana kama hivi kifo kimemkuta ikiwa bado hatujapatana,
namuombea lakini pia anisamehe huko aliko,” alisema Irene.
0 comments: