ANGALIA KLABU ZILIZOTOA WACHEZAJI WENGI KWENDA KOMBE LA DUNIA

Homa ya kombe
la dunia inazidi kupanda zikiwa zimebaki takribani wiki zipatazo nne
kabla ya michuano hiyo haijaanza kutimua vumbi kwenye viwanja tofauti
nchini Brazil. Timu zote 32 tayari zimeshatangaza vikosi vyao kwa ajili
ya michuano hiyo.
Katika
vikosi vyote vya timu za taifa vilivyotajwa kwa ajili ya kombe la dunia
Brazil 2014 – Klabu ya Bayern Munich ndio inaoongoza kwa kutoa
wachezaji wengi – imetoa wachezaji 17 watakaowakilisha mataifa
mbalimbali kwenye kombe la dunia.
Klabu ya
Manchester United inashika nafasi ya pili baada ya Bayern na nafasi ya
kwanza EPL kwa kutoa wachezaji wengi walioitwa kwenye timu za taifa
zitakazoshiriki michuano ya kombe la dunia – UNITED imetoa wachezaji 16.
Chelsea
ya England imeshika nafasi ya 3 kwa kutoa wachezaji 15, Napoli 14,
Barcelona na Real Madrid wametoa wachezaji 13 kila timu, Juventus imetoa
wachezaji 13.
0 comments: