VIJUE VITU VITANO UNAVYOHITAJI KABLA YA KUANZA BIASHARA
1. Unahitaji bidhaa au huduma nzuri na bora
Biashara yoyote haina kitu bila kuwa na bidhaa au huduma. Unahitaji kitu cha kuuza, kama ni bidhaaa halisi, huduma au ushauri. Hivyo unahitaji kutumia muda mwingi kufanya uchunguzi na utafiti ili utoke na kitu gani cha kuuza. Biashara nyingi zinashindwa kwa sababu hakuna anayeuza kitu chake mwenyewe. Fikiria watu wanaotengeneza tovuti huuza kitu ambacho wamekichukua sehemu nyingine. Jaribu kuwa mbunifu na bidhaa unayokuja nayo, lasivyo utaingia sokoni na kukatishwa tamaa kwani utakuta bidhaa ipo tayari. Usiige biashara ila unaweze kuboresha matengenezo, kutoa kitu kizuri zaidi au kubadilisha kabiha muonekano wa hicho kitu.
2. Unahitaji timu nzuri ya watu wako
Hata
kama ni biashara ndogo, unahitaji watu unaofanya nao kazi kama
umewaajiri au mnafanya biashara pamoja au wanakufanyia kazi kwa muda.
Hao wote wanatakiwa wawe ni wazuri wa kufanya kazi inayotakiwa kwa ubora
na wakati sahihi. Wawe ni watu wabunifu, wenye uwezo wa kufikiria
kibiashara na kutafuta wateja wa bidhaa yako.
3. Unahitaji teknolojia sahihi
Unahitaji
kuwa na teknolojia inayokwenda na wakati, wateja hawatanunua kwa sababu
kimetengenezwa Tanzania. Watanunua kwa sababu kina ubora unaohitajika,
achana na siasa za uzalendo, wekeza kwenye teknolojia sahihi na utoe
huduma kwa ubora wa hali ya juu.
4. Unahitaji ushauri mzuri kwenye mambo ya kodi
Unapoanza
biashara unakuwa unahitajika kulipa kodi za mapato kwa serikari husika,
hivyo unatakiwa kujua namna ya ulipaji wake. Kabla ya kufanya chochote
kwenye kodi tafuta mshauri mzuri anayejua sheria za kodi na anajua
utaratibu mzuri ambao hautakuletea matatizo.
5. Unahitaji nidhamu ya kazi
Kama
unavyofanya kazi na mtu mwingine unakuwa na watu wengi wamewekeza kwako
hivyo kila siku kazi inatakiwa ifanyike. Ndio maana kuna meneja huyo
usiyempenda ambaye kila
0 comments: