NDEGE NYINGINE YA MALAYSIA YATUA HONG KONG KWA HITILAFU YA UMEME!! ANGALIA HAPA
Wakati bado juhudi zinaendelea bila mafanikio za kuitafuta ndege ya
Malaysia Airlines aina ya Boeing 777-200 iliyopotea March 8 mwaka huu
ikiwa na abiria 239, ndege nyingine ya shirika hilo imelazimika kutua
Hong Kong, china kwa dharula baada ya hitilafu za umeme kujitokeza ikiwa
safarini.Maafisa wa shirika hilo wameiambia CNN mapema leo kuwa ndege
hiyo aina ya Airbus A330-300 iliyokuwa ikitokea Kuala Lumpur kuelekea
Incheon, Korea Kusini ililazimika kubadili njia na kwenda kutua kwa
dharula Hong Kong baada ya wafanyakazi wa ndege hiyo kugundua hitilafu
katika genereta inayozalisha umeme wa kawaida wa ndege hiyo.Kuala Lumpur
ndio uwanja wa ndege ilipotokea ndege ya shirika hilo iliyopotea ambayo
hadi sasa bado haijaonekanekana.Hata hivyo maafisa hao wameongeza kuwa
pamoja na hitilafu iliyojitokeza lakini umeme uliendelea kuzalishwa
kupitia power unit ndogo ya ndege hiyo.SOURCE: MAIL ONLINE
0 comments: