ANGALIA PICHA MZEE WA MIAKA 60 AUAWA KINYAMA KWA TUHUMA ZA USHIRIKINA WILAYANI MAKETE,
Daktari
Luvanda kutoka hospitali ya wilaya ya Makete akionesha majeraha ya
kichwa cha mwili wa marehemu yanayohisiwa kupelekea kifo chake.
Polisi
kutoka kituo cha Tandala na Makete wilayani wakichukua taarifa za mauaji
hayo kwenye shamba ulipokutwa mwili wa marehemu.
Askari
akizungumza na wananchi waliofika eneo la tukio na kuwaonya kuacha tabia
ya kujichukulia sheria mikononi pamoja na kushirikiana na jeshi hilo
kuwapata watuhumiwa wa mauaji hayo.
Mkazi
wa kijiji cha Masisiwe kata ya Ukwama Wilayani Makete Mkoani Njombe
amefariki Dunia baada ya kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani na
mguuni na mtu/watu wasiojulikana mwishoni mwa wiki iliyopita
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo kwa niaba ya mkuu wa polisi wilaya, Mrakibu
mwandamizi wa Polisi ambaye pia ni afisa upelelezi Wilaya ya Makete
Bw.Gozbert Komba amesema walipokea taarifa ya mauaji hayo kutoka kwa
uongozi wa kijiji hicho na kumtaja marehemu kuwa ni Masori Sanga(60)
mkazi wa kijiji cha Masisiwe Kata ya Ukwama Wilayani Makete
Bw.
Komba amesema kuwa marehemu huyo aliuawa usiku wa kuamikia Ijumaa wiki
iliyopita na watu wasiojulikana kwa imani za kishirikina kwa kuwa
marehemu alikuwa mzee na pia kwa mujibu wa maelezo ya mashuhuda wa tukio
hilo waliohojiwa na polisi
Pia
amesema mpaka sasa Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi kwa ajili
ya kuhakikisha wahusika wote wa tukio hilo wanakamatwa kwani kitendo
walichokifanya ni cha kinyama na baada ya tukio hilo muuaji/wauaji hao
walitokomea kusiko julikana
Bw.Komba
amekemea vikali suala la wananchi kujichukulia sheria mkononi wilayani
hapo na kuwaomba wananchi wasiwe na tabia hizo za kuwaua wazee kwa
imani za kishirikina na kuwataka watii sheria bila shuruti ili kuishi
kwa Amani katika wilaya yao na nchini kwa ujumla
Mwili
wa marehemu ulikutwa kwenye shamba la mahindi ukiwa na majeraha sehemu
za kichwani na mguuni ambayo yanadhaniwa kusababisha kifo chake, baada
ya watu kupita eneo hilo na kuukuta mwili huo
katika
kipindi cha hivi karibuni wilayani Makete kumekuwa na matukio ya mauaji
kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo wivu wa kimapenzi na imani za
kishirikina jambo linalotia doa wilaya hiyo kutokana na ongezeko la watu
kuchukua sheria mikononi kwa kuwaua watuhumiwa wa matukio mbalimbali
Habari/picha na Edwin Moshi, Eddy Blog.
0 comments: