WATU 28 WAUAWA NCHINI CHINA KISA NA MKASA SOMA HAPA KUJUA
Nchini Uchina, kundi moja la watu waliojihami kwa visu limewauawa
takriban watu 28 katika kituo kimoja cha treni kusini magharibi mwa mji
wa Kunming. Kituo cha habari cha Xhinua kimesema kuwa zaidi ya watu mia
moja walijeruhiwa.
Baadhi ya majeruhi katika shambulio hilo wakiwa hospitali.
Mashahidi
wamesema kuwa washambuliaji hao waliovalia nguo nyeusi,waliwavamia
abiria waliokuwa wakingojea kuabiri treni na kuwakatakata huku wengine
wakiwadunga visu wale walioshindwa kukimbia kwa kasi.
Miili ya watu waliouawa katika shambulio hilo.
Kulikuwa
na takriban washambuliaji 10..Polisi waliwapiga risasi na kuwaua
washambuliaji 5 huku wakiwasaka waliosalia. Shirika la habari la Xhinua
limewalaumu watu wanaopigania kujitenga katika mkoa wa Shinjiang kwa
tukio hilo.
Baadhi ya mizigo iliyoachwa eneo la tukio.
0 comments: