WAISLAMU WALAANI KUCHANWA KWA KORANI HUKO MAURITANIA
Mamia ya
waislam wamefanya maandamano katika mji mkuu wa wa Mauritania
Nouakchott, baada ya kuenea kwa taarifa kuwa Koran imechanwa msikitini. Imam
ameripoti kuwa watu wanne waliokuwa wamefunika nyuso zao waliingia
msikitini , wakachana nakala za Koran na kuzitupa chooni. Polisi
walifyatua mabomu ya kutolea machozi kutawanya umati wa watu waliokuwa
na jazba, na mtu mmoja aliuawa, duru za polisi zilieleza.
Mauritania ni taifa la kiislam , likiwa na idadi ndogo ya wakristo.
Imekuwa
mshirika muhimu wa nchi za magharibi katika kampeni dhidi ya al-Qaeda na
makundi mengine ya wanamgambo yanayoendesha harakati katika kanda hiyo .
Mwandishi wa
habari Hamdi Mohamed El Hacen aliyeko mjini Nouakchott anasema
waandamanaji walichoma vizuizi na maduka mengi na masoko yalifungwa jana
siku nzima.
Mamia ya
waandamanaji walikusanyika kati kati mwa mji mkuu na nje ya msikiti
wakipaza sauti "Mungu ni mkuu" wakidai wahusika wakamatwe na kuhukumiwa
kifo kwa madai ya kukufuru uislam, alisema.
Chanzo - BBC Swahili
0 comments: