UNATAFUTA KUPENDWA NA WALE WANAOKUZUNGUKA? BASI SOMA HAPA
Ni
moja ya mawazo na fikra ndani ya watu wengi, kama hujawahi kuwa kwenye
hali hiyo ninaweza kusema una bahati. Kwanini watu hawanipendi? Ni swali
ambalo mara nyingi kila mtu hujaribu kujiuliza labda moja kwa moja au
kwa kufanya vitu ili aweze kukubalika na watu fulani.
Inawezekana
wewe ni mwandishi wa makala fulani, au mwimbaji, au mfanya biashara au
mfanyakazi kama wengine , bosi, mfagiaji hata kama ni mlinzi. Kama
ilivyo kwa mtu yeyote mimi pia ninapenda nipendwe, hiyo ni kibinadamu
kabisa na hakuna tatizo kuhusu hilo. Tatizo ni pale unapotaka watu
wakupende huku ukijaribu kufanya hiki na kile, sio kazi yako kumshawishi
mtu akupende kama uko kazini au nyumbani, kwenye biashara na sanaa
nyingine. Ukijikuta wewe unajaribu kushawishi watu ili upate marafiki,
wafuasi, inawezekana hufanyi mambo yako sawasawa.
Badala
ya kuwambia watu au kuwashawishi wakupende, zingatia kazi na majukumu
yako, yafanye vizuri na kwa ustadi mkubwa. Utakapofanya kazi zako
vizuri, mfano labda wewe ni mwandishi unahitaji kuandika makala zenye
kuleta tija kwa wasomaji wako huku ukionyesha weledi wa hali ya juu au
wewe ni mpishi wa mgahawa hapo mtaani unachotakiwa kufanya ni kupika
chakula kizuri na kwa kuzingatia afya bora utajikuta watu wanakupenda na
kuipenda kazi zako.
Hakuna
bia utakazomnunulia mtu zinazoweza kumshawishi akupende, siku hizo bia
zikiisha na yeye anaondoka, Si kwa kumtoa na kumpeleka kula hoteli
nzuri au kwa kufanya vituko kujaribu kutafuta ushawishi watu wakupende.
Pale unapojaribu kufanya watu wakupende ndipo unapoweza kujiharibia au
kuharibu maisha yako na taaluma yako, fanya kitu sahihi na watu sahihi
na mwishowe utapata watu sahihi wanaokupenda na kukuthamini.
Usijiunge
na kundi fulani la watu ili uonekane unakubalika, bali fanya
kinachostahili kufanywa na watu watakukubali. kwa kufanya hivyo
utapotesha wanafiki wengi na kupata marafiki na watu wakweli wanaopenda
kazi yako, jitihada zako na bidhaa zako. Kama unahitaji kung’ara
utang’ara tu kwakuwa unafanya kitu sahihi.
Je
unahitaji watu wakupende na kupenda kazi zako mwezi huu? Dumisha ubora
wa kazi zako ikiwezekana ongeza ubora, fanya kazi kwa juhudi, kama ni
mwanamuziki ungeza ubunifu katika kazi zako na usiambatane na watu
wasiokua na tija kwenye taaluma yako.
Uwe na wiki njema yenye mafanikio.
0 comments: