SHEREHE ZA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI ZILIZOANDALIWA NA CSO GENDER COALITION ZAFANYIKA LEO KWENYE VIWANJA VYA CHUO KIKUU CHA UDSM
Kutoka
kushoto ni Miss Tanzania 2013 Happy Watimanywa , Dk. Agnes Nyomola
kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam ambaye ni Mtaalam wa mambo ya
Sayansi, na Specioza Rweyemamu ambaye ni Ispecta katika mambo ya anga
katika Mamlaka wa usafiri wa Anga Tanzania, ambao ndio walikuwa wasemaji
katika sherehe hizo
Specioza
Rweyemamu ambaye ni Ispecta katika mambo ya anga katika Mamlaka wa
usafiri wa Anga Tanzania akizungumza na wanafunzi pamoja na wageni
waalikwa mbalimbali hasa wanafunzi na kuwaasa kuwa wanatakiwa kuwa mfano
wa kuigwa katika jamii na kusoma kwa bidii kwani hakuna kisicho
wezekana kila mtu anaweza, pia amewasihi wasichana hasa wadogo kupenda
kusoma zaidi ili waje kuwa viongozi wa baadae.
Wakili
wa Mahakama Kuu Modesta Mahiga akizungumza na wanafunzi waliofika
katika Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Chuo Kikuu Dar es salaam na
kuwahimiza wanafunzi hasa wakike wanaokuwa wasikimbilie katika mambo
makubwa lakini wakazane na masomo ili kupata kufanikiwa zaidi.
Miss
Tanzania 2013 Happy Watimanywa akiongea na wanafunzi, alisisitiza sana
wanafunzi wenzake wa kike kuwa wanatakiwa kusoma kwa Bidii ili kuweza
kuja kufanikiwa katika mambo yao ya mbeleni, aliongeza kuwa mtoto wa
kike ndio taifa la kesho na kiongozi wa kesho hivyo ni lazima wakazane
sana katika masomo yao na kuichukulia siku ya leo kama changamoto na
chachu kwao ya kujibidisha zaidi.
Jane
Mrema Mshauri wa Jinsia kutoka Shirika la Plan International akielezea
nia yao kubwa ya kushiriki katika Sherehe hizo Leo.
Gloria
Chambo mwanachama wa chama cha Muunganiko wa mashirika yasiyo ya
Kiserikali ambaye ndiye alikuwa mshereheshaji wa Siku hiyo ya wanawake
akizungumza Jambo wakati wa Sherehe hizo na kuongoza ratiba hiyo.
Baadhi
ya wanafunzi wa shule mbalimbali kutoka Jijini Dar es salaam wakiwa
wanafuatilia mambo mbalimbali yanayo endelea wakati wa sherehe hizo
Hawa
ni wanafunzi wa Chuo cha ufundi kwa watu wenye ulemavu walemavu wa
jumla, wakiwa wanafuatilia kwa umakini kinacho endelea uwanjani hapo
Msichana
mfupi Mbele ni Mwanafunzi wa Chuo cha ufundi kwa watu wenye ulemavu
Jovina Vedastus ambaye ni Fundi wa Ushonaji na utengenezaji wa Batiki
akicheza muziki ambapo alikonga nyoyo za watu wengi kwa umahili wake huo
katika kucheza
Wasemaji wakifurahia Burudani mbalimbali zinazo endelea
Wanafunzi
wa Chuo cha ufundi kwa watu wenye ulemavu walemavu wa jumla, hapa
wakiwa viziwi, wasio ona, wenye ulemavu wa Miguu , mikono mapoja na
Matatizo mengine wakiwa wanatumbuiza na burudani ya aina yake ambapo
watu wengi walivutiwa sana na kufurahishwa.
Banana Zoro akitoa Burudani ya uhakika pamoja na Bendi yake wakati wa maadhimisho hayo.
Mwakilishi
kutoka OXFAM ambao pia ni wanachama wa chama cha Muunganiko wa
mashirika yasiyo ya Kiserikali Afisa utetezi wa haki za kiuchumi OXFAM
Bi.Mkamiti Mgawe akifunga Rasmi sherehe hizo na kuwashukuru wote
waliofika katika katika sherehe hizo zilizofanyika katika viwanja vya
Chuo Kikuu jijini Dar es salaam leo.
Hili
lilikuwa ni Tukio la Aina yake ambapo Miss Tanzania 2013 Happy
Watimanywa alipo vamiwa na wanafunzi kutoka shule mbalimbali za
Sekondari Jijini Dar es salaam wakiomba awasainie katika Madaftari yao
kama kumbukumbu ya kwamba na wao walisha wahi kumuona Mrembo huyo, Hapa
akiwa anasaini katika Baadhi ya Madaftari hayo.
0 comments: