RAIS KENYATTA APUNGUZA MSHAHARA WAKE NA SAFARI ZA NNJE
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta
Taarifa
ikufikie kwamba Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametangaza kupunguza
mshahara wake na wa Makamu wake William Ruto kwa asilimia 20 na mshahara
wa Mawaziri utapunguzwa kwa asilimia 10.President mwenyewe amesema hii
ishu nzima iliafikiwa kwenye mkutano na baraza la Mawaziri uliofanywa
kwa siri ambapo amekaririwa akisema ‘tukizingatia hali ya kupanda kwa
garama mimi na makamu wangu tunachukua hatua ya kupunguza mshahara wetu,
makatibu wakuu wa serikali na makatibu wasaidizi nao wamekubali
asilimia kumi kukatwa kwenye mishahara yao kuanzia sasa’.
‘Kingine
ni kwamba tutaandaa mkataba mpya wa kusafiri ambao utafuta safari za nje
ya nchi isipokua zitabaki zile zenye umuhimu tu, serikali yangu
inampango wa kupunguza matumizi yanayojirudia na ambayo hayaongezi
umaana wowote kwenye ufanyaji kazi’
0 comments: