RAIS KIKWETE ATEMBELEA VIKOSI VYA JWTZ VYA KOMANDO NA UHANDISI MEDANI MKOANI MOROGORO MACHI
Waziri
wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi (Mb),
(Mwenye kaunda suti nyeusi) akisalimiana na Makamanda wa JWTZ mara baada
ya kupokelewa na Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Luteni Jenerali
Samuel Ndomba (Aliyesimama kulia kwa Mhe. Waziri) muda mfupi kabla ya
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete kuanza ziara ya kutembelea vikosi ya JWTZ vya
Makomando na Wahandisi wa Medani Mkoani Morogoro. Nyuma ya Mhe. Waziri
ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na JKT, Bibi. Mwitango Rose
Shelukindo.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akiwasili kwenye Kikosi cha Komando kuanza ziara yake ya
kujionea hali na utimamu wa vikosi vya JWTZ Mkoani Morogoro.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akipokea taarifa ya Utawala na Utendaji kivita kutoka kwa
Mkuu wa Kikosi cha Komando wakati wa ziara yake.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akipewa maelezo kwa kutumia mchoro kuonesha mzunguko
mzima wa maeneo atakayotembelea katika kikosi cha Komando.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akiangalia kupitia kilengeo maalum kinachotumiwa kwenye
silaha na makomando kulengea shabaha.
Makomando
wakimuonesha Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (hayuko pichani) mapigano bila
shilaha wakati wa ziara yake.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akifurahia mapambano ya kareti, taikondo na judo
yaliyokuwa yakioneshwa na makomando wa JWTZ (Hawamo pichani).
Komando
wa JWTZ akionesha uwezo wa kukwepa mapigo ya risasi za adui kwa kupita
juu ya mapigo hayo kwa kutumia kamba na kisha kuendelea na jukumu
alilopewa.
Kamanda
wa Kikosi cha Uhandisi wa Medani akitoa taarifa ya Utawala na Utendaji
Kivita kwa (Hayupo pichani) mara baada ya Kikosi hicho kutembelewa.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akifafanua maeneo kadha ambayo Wahandisi Medani wa JWTZ
wamefanya kazi nzuri kurejesha miundombinu ya reli, barabara na madaraja
hata pale ambako Mamlaka za Kiraia zimekuwa na maoni kuwa kazi hizo
zingehitaji muda mwingi zaidi.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akipewa maelezo kuhusu moja ya mitambo mipya inaotumiwa
na Wahandisi medani kusafisha maji chumvi na baridi na kuwa maji safi na
salama inayomilikiwa na Kikosi cha Uhandisi Medani.
akipata maelezo kuhusu baadhi ya mitambo mipya ya kutengeneza barabara katika Kikosi cha Uhandisi Medani.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akivuka juu ya daraja jipya la medani lililojengwa
kumuonesha uwezo wa Wahandisi Medani wa JWTZ kuendelea kusaidia
usafirishaji wa zana na vifaa hata pale madaraja ya kudumu
yanapoharibiwa kwa namna yoyote ile.
Picha/habari na Luteni Kanali Juma Nkangaa Sipe, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ulinzi na JKT
Picha/habari na Luteni Kanali Juma Nkangaa Sipe, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ulinzi na JKT
Amiri
Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,Rais Jakaya Kikwete amefanya Ziara ya siku moja
katika Vikosi vya Jeshi la Wanannchi wa Tanzania (JWTZ) vya Komando na
Uhandisi Medali vilivyopo Mkoani Morogoro.
Akizungumza
katika kikao maalum na wakuu wa vikosi,Rais Kikwete amesema
ameridhishwa sana na utimamu wa vikosi hivyo kimafunzo na pia amehidi
kukiongezea vifaa zaidi kikosi cha Uhandisi wa Medani ili kiweze
kupambana na majanga hapa nchini.
Rais Kikwete pia amelitaka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kubuni mikakati ya kuondokana na Makazi ya muda.
Katika
ziara hiyo,Rais aliambatana pia na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel
Bendera, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Wakuu wa Kamandi,
Wakuu wa Matawi Makao Makuu ya Jeshi, Makamishna Wizarani na Wajumbe wa
Mabaraza ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya na Mkoa wa Morogoro.
0 comments: