HIVII UNAHITAJI SHILINGI NGAPI ILI UWE NA FURAHA?
Je
ni fadha kiasi gani inaweza kununua furaha yako? Kitu kikubwa ambacho
kitapima furaha yako ni kuridhika na kufanikiwa kwa kile unachokifanya
kazini kwako au kwenye biashara yako na maisha uliyonayo katika jamii
inayokuzunguka. Fedha ni uwezo wa kununua vitu na mali, bali haiwezi
kununua furaha ya mtu.
Unapoweza
kupata fedha ya kujikimu, mambo kama chakula, Mavazi, malazi, maji na
umeme vingi vinavyokuja zaidi ya hapo ni ziada. Na vijana na watu wengi
tumekuwa tukichukulia fedha kwa mtazamo tofauti na kujikuta tunafanya
mambo ambayo ni magumu tukifikiria kwamba tunatafuta furaha. Tumeendelea
kufanya kazi muda mrefu huku tukishindwa kujenga familia kimaadili,
mahusiano na upendo kwa kisingizio cha kutafuta pesa na furaha zaidi.
Kila kitu kinapoondoka kama ni mali na utajiri kinachobakia ni watu,
hivyo jenga uhusiano mzuri na watu wanaokuzunguka na furaha unayoitafuta
kwenye fedha haitakusumbua tena.
Unapochagua
kazi kulingana na kiwango cha mshahara ukitegemea kuwa na furaha zaidi,
unajidanganya kwa kuwa hautaridhika na fedha hiyo. Unahitaji kuridhika
kwa kile unachokifanya na utaweza kupata furaha unayoitafuta.
Hakikisha
una mahali pa kulala, umekula, umevaa, una maji na umeme na utakuwa na
furaha, tatizo ni kufuata mkumbo wa watu wengine wanaishije. Tunaporudi
kwenye swali la msingi, unahitaji shilingi ngapi ili uwe na furaha?
Inategemea na jamii uliokulia na namna walivyopotosha neno furaha, hivyo
kuleta matatizo katika kufikiri kwako na jamii inayokuzunguka. Furaha
yako haitapatikana kwa kulazimisha kila mtu akuogope kwa fedha na mali,
au dini, au elimu yako. Jitambue na uheshimu kwamba furaha inapatikana
ndani yako mwenyewe endapo tu uwezo wako wa kufikiri utafikiri vizuri.
Maisha zaidi ya fedha, ni mtu kujitambua kwa kuwa thamani ya utu wako ni zaidi ya fedha unayofikiri itakupa furaha.
0 comments: