MASKINI TAMTHILIA YA SIRI YA MTUNGI YAAMBULIA PATUPU TUZO ZA MOVIE AFRICA

Watanzania tulifurahi kwa habari kuwa Tamthilia yetu ya Siri ya Mtungi imechaguliwa kuwania Tuzo Saba katika  tuzo za Africa Magic Movie Awards 2014’ Tuzo hizo zilifanyika jumamosi hii lakini kwa Bahati Mbaya Haikuweza kupata Tuzo hata Moja...

Kinachoumiza zaidi ni hata katika kipengele ambacho ilikuwa ni lazima Siri ya Mtungi ishinde cha Best Indigenous Language Movie/Series (Swahili) kilichukuliwa na Wakenya, Njoki Muhoho – Mama Duka.

Inatia wasiwasi kidogo kwakuwa hakuna fundi wa Kiswahili duniani kumzidi mswahili mwenyewe wa Tanzania. Inapofikia hadi Mkenya anachukua kile tunachokiweza zaidi, ni ishara kuwa tunahitaji kujitafakari tunakosea wapi. Ni kweli Wakenya ni mafundi wa Kiswahili kuliko sisi? Tatizo ni nini?

“Nadhani kilichopelekea Siri ya Mtungi kukosa tuzo ni vitu viwili, kwanza tabia ya Watanzania sisi kutopenda kupiga kura, hiyo ndio tatizo la kwanza, lakini pili crew ya Siri ya Mtungi yenyewe haikuwa na nguvu kubwa kwenye kushawishi wadau katika upigaji kura. All in all jamaa wako vizuri I hope next year tutafanya vizuri. Nadhani pia waandaaji wa Tuzo zozote Tanzania wamejifunza nini maana ya Tuzo,” anasema King David, mtangazaji wa Kings FM ya Njombe.

David yupo sahihi kwa mmoja. Ni kweli kabisa, lawama ije kwetu sisi wenyewe Watanzania tulioshindwa kuwa wazalendo kwa kuwapigia kura Siri ya Mtungi washinde, lakini mfumo wa tuzo hizo ulikuwa tofauti kidogo. Kulikuwa na jumla ya vipengele 27 na ni vipengele 9 tu kati ya hivyo ndivyo vilikuwa vya watazamaji kupiga kura na kuchagua mshindi.

Kwenye vipengele vilivyokuwa vikipigiwa kura (Votable Categories) Siri ya Mtungi ilikuwa imetajwa kwenye kipengele kimoja tu ambacho ni BEST ACTOR IN A DRAMA alichokuwa ametajwa ‘Juma Rajab Rashid’ aka Cheche.

Vipengele vingine 6 ambavyo Siri ya Mtungi ilikuwa imetajwa, vilikuwa ni vile ambavyo jopo la wataalam limekaa na kuchagua mshindi linayemuona ni bora katika kipengele husika. Mara nyingi katika mfumo wa aina hii, yote yanaweza kutokea na upendeleo na mapenzi ya nchi fulani fulani yanaweza kuchukua nafasi.

Kipengele cha kupigiwa kura alichokuwa ametajwa Cheche, kilikuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa Majid Michel ( Somewhere in Africa), Hlomla Dandala ( Contract), Majid Michel (House of Gold) na Tope Tedela (A Mile from Home). Ili Cheche ashinde, alitakiwa kupigiwa kura nyingi sana, na kwakweli haikuwa rahisi kuwazidi waigizaji wa Nigeria ama Afrika Kusini katika kipengele hiki japo yote yanawezekana.

0 comments:

Copyright © 2013. MSANGIBIN ALLY - All Rights Reserved
Customized by: MSANGIYUSUPHALY | Powered by: KIINICHAHABARI
Designed by: http://kiinichahabaribongo1.blogspot.com/