JIHADHARI DHIDI YA PESA NA MATUMIZI YA PESA IWE YA NOTI AU SARAFU .. UNAJUA NI KWA NINI SOMA HAPA
Wataalamu wa afya na tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa fedha hasa sarafu zina madhara kwa afya ya binadamu kutokana na mzunguko wake ulivyo mkubwa.
Kwa mfano, tunaambiwa kuwa fedha inatembea kuliko pengine anavyotembea mtumiaji wake. Haichagui wa kuitumia,
wanaitumia wenye akili timamu na hata wasiokuwa nazo,
hivyo inategemea mtu wa mwisho aliitumia vipi kwa kuwa kuna watu wanajifutia jasho noti bila kujali kuwa atampa mtu mwingine.
Kuna baadhi ya watu wanahifadhi fedha hizo zikiwamo sarafu na noti kwenye sehemu zisizo salama. Tunaambiwa fedha zina madhara, wakati mwingine zinaweza kusababisha maradhi kwa kuwa zinabeba vimelea vya magonjwa
kwa urahisi kutokana na kuwa katika mzunguko siku zote.
Uchunguzi umebaini kuwa fedha za noti na zile za sarafu huweza kukusanya na kusambaza vimelea vya magonjwa hatari kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
Vimelea hivyo vina uwezo wa kusababisha maradhi kama ya ngozi, kuharisha, magonjwa ya fizi, homa za vipindi na
mengineyo. Kibaya zaidi magonjwa mengi huchukua muda hadi kujitokeza na yanapojitokeza huwa tayari yameshaleta madhara ambayo yameingia mwilini taratibu bila mhusika kujua.
Pamoja na kubeba vimelea hivyo, lakini fedha pia inao uwezo wa kubeba sumu kutoka eneo moja kupeleka lingine kulingana na mzunguko wake.
Kwa hiyo, ushauri wangu kwa wauza chenji na wateja wao ambao kazi yao kubwa ni kushika fedha baadhi wamekuwa wakijisahau na kula huku wakiwa nazo mkononi.
Wanashauriwa waache tabia hiyo.
0 comments: