JE UNAJUA MUONEKANO WA MPENZI MWENYE MAPENZI YA KWELI KWAKO......SOMA ZAIDI HAPA


Ni matumaini yangu kua umzima wa afya tele na nijambo jema pia kumshukuru Mungu kwa kukujalia hii afya njema na mpaka sasa tuna kutana tena katika mada nyingine muhimu katika mahusiano na maisha.
Mada ya leo inahusu utambuzi wa mtu mwenye mapenzi ya kweli kwako, hii inatoka na migogoro mingi na ndoa nyingi za siku hizi kuvunjika pasipo kuwa na sababu ya muhimu, kwakuligundua hilo basi nikaona ni vyema tushirikishane haya machache ambayo ninayo ili tusije kujutia maamuzi yetu baadae tutakapo fanya uchaguzi pasipo kuangalia vigezo na upendo wa dhati.

Kuna watu wanajiuliza kua hivi nitamjuaje mwenzi anayenipenda kwa dhati?Rafiki zangu naomba niseme kua hakuna kanuni ya moja kwa moja ya utambuzi wa mapenzi ya kweli....
Inawezekana kwa mpenzi huyu ikatumika kanuni moja,na kwa mwingine ikatumika kanuni nyingine tofauti kabisa,ndivyo mambo yalivyo.Lakini yapo mambo ya msingi ya kuangalia kwa mpenzi wako ukagundua kuwa anamapenzi ya dhati kwako kama ifuatavyo:-
 *  mwenye kukupenda atajitoa kwako.
*  ni msikivu na mtulivu kwako na hapendi kukuudhi.
* ukiondoa suala la umakini ambalo ni tabia ya mtu suala la kujali na kua    huruma linpewa kipaumbele na mtu mwenye mapenzi ya kweli.
* atakua mkweli kwako tangu awali na hatapenda mapenzi ya uchochoroni.
*  atakua radhi mahusiano yenu yajulikane na yeyote kwa sababu kwa sababu ana jiamini kwamba anakupenda .
* mawasiliano ni kiunganishi muhimu,hata kama yuko busy kiasi gani,mawasiliano atayadumisha kwa sababu huongeza chachu huongeza chachu kwenye mapenzi nakuwafanya muwe karibu....

kumbuka kua hizo ni baadhi tu ya sifa ambazo mpenzi mwenye mapenzi ya kweli anatakiwa kua nazo....

Ni MATUMAINI YANGU KUA UTAKUWA ANGALAU UMEPATA CHOCHOTE KITU HAPO
....sasa ukiangalia vigezo hivi unaweza kugundua kua uliyenaye ana Mapenzi ya   kweli na wewe au hana
....ila angalizo ni kwamba hata ma playboy na playgirl wanaweza kuja na muonekano kama huo sasa akili kwa kichwa...

0 comments:

Copyright © 2013. MSANGIBIN ALLY - All Rights Reserved
Customized by: MSANGIYUSUPHALY | Powered by: KIINICHAHABARI
Designed by: http://kiinichahabaribongo1.blogspot.com/