JE KWANINI NI MUHIMU WAKATI MWINGINE KUWA NA MTU WA KUKUSHAURI
Maisha
yanavyokwenda unahitaji kuwa mtu mwangalifu na nani yuko karibu yako.
Unahitaji mshauri wa mambo yako ya karibu, kama biashara, Maisha kwa
ujumla, ndoa, taaluma na hata Kiroho. Kuwa na mshauri ni dhana ambayo
watanzania wengi hatujaizoea na hufikiri tunaweza kufanya kila kitu,
lakini mambo yako yanakuwa bora zaidi unapokuwa na mshauri mwenye uzoefu
mkubwa kuliko wewe na aliyekutangulia kwa namna fulani.
Fikiria kuhusu wewe mwenyewe, Je unahitaji mshauri?
Watu
wengi huwa tunajitahidi kujilinda ili tusijulikane makosa yetu au
udhaifu tulionao kwenye biashara, taaluma, ndoa na hata maisha ya
kawaida. Ukweli ni kwamba bado hujafika kiwango unachotakiwa kufika,
unahitaji ushauri hasa kwa kile unachofanya. Ikiwa wewe ni kiongozi
tafuta kiongozi bora kuliko wewe apate kukusaidia mambo kadha wa kadha.
Mshauri
wako anahitajika kuwa mtu mwenye uadilifu mkubwa, aliyefanikiwa, mwenye
hekima na upeo mkubwa kimaisha na hata kifikra. Si kila unayemwona
mbele yako anaweza kukushauri hata kama ni mkubwa kuliko wewe, hapa
sizungumzii ndugu, nazungumzia mtu ambaye yuko tayari kukwambia ukweli
na kukusaidia.
Tumekuwa
na hulka ya kuwaheshimu watu fulani labda kwa sababu ya madaraka yao,
fedha na nguvu walizonazo lakini inapokuja suala la maisha yako binafsi
kazini, nyumbani , kwenye uongozi na biashara unahitaji mtu mwenye
akili timamu.
Mtu
ambaye ndoa yake inayumba hawezi kukusaidia ndoa yako kiushauri, hiyo
sahau. Mtu ambaye biashara hajui au hajawahi kufanya biashara usitegemee
kuwa anaushauri wa kukuza biashara yako. Huweza kukaa chini ya mkwaju
halafu unategemea kuvuna maembe. “Fikiri na chukua hatua”
Fanya Uchunguzi kuhusu mtu anayetakiwa kukushauri.
Hapa
ndipo unaweza kuyakoroga mambo, watu wengi tunaangalia uwezo wa
kifedha, madaraka na umaarufu, sahau hayo yote angalia uadilifu, ndoa
yake ina msimamo au yeye mwenyewe ana msimamo au ni kiruka njia? Kama ni
mfanyabiashara fanya uchunguzi wa biashara zake, anafanya biashara na
nani, utu wake ukoje na hali yake ya kiroho imekaaje? Je ni muumini
mwadilifu au haeleweki? kama haeleweki hata maadili yake hayaeleweki.
Ukisharidhika
na uchunguzi wako, chukua hatua ya kumwomba kuwa mshauri wako kwenye
jambo ambalo unaona anafaa. Akikubali endelea naye akikataa endelea
kutafuta mtu mwingine. Wakati wa kuishi kufuata mkumbo umekwisha, ni
sawasawa na kuishi maisha ya wengine na maisha yako hujawahi kuishi.
Nitafurahi kusikia kutoka kwako ndugu msomaji wetu. Siku jema!
0 comments: