Barcelona wamepoteza mchezo mmoja tu kati ya 18 ya mwisho waliyocheza katika hatua ya mtoano ndani ya dimba la Camp Nou kwenye michuano ya Champions League (0-3 v Bayern Munich msimu uliopita).
Kati
ya michezo 30 ya hatua ya mtoano ya michuano ya Champions League,
Barcelona wamepoteza michezo miwili tu kwa angalau mabao yasiyopungua
mawili (0-2 v Real Madrid in April 2002 na 0-3 v Bayern Munich in May
2013).
Ni
klabu moja tu ya kiingereza iliyoweza kufanikiwa kuifunga Barcelona
katika dimba la Camp Nou kwenye Champions League (kwenye michezo 17):
Liverpool mnamo February 2007 (1-2).
Mechi 3 za mwisho za Champions League ndani ya dimba la Camp Nou zimezalisha mabao 13.
Manchester City hawajawahi kushinda dhidi ya klabu ya Uhispania kwenye michuano ya Champions League.
Manchester
City wameshinda mechi zao tatu za ugenini kwenye Champions League msimu
huu, ukiwemo ushindi wa 3-2 dhidi ya mabingwa watetezi Bayern Munich.
Manchester
City wameweza kuzuia wavu wao kuguswa mara moja katika mechi 13 za
mwisho za Champions League (ushindi wa 3-0 dhidi ya Viktoria Plzen)
Barcelona
ndio timu yenye rekodi nzuri zaidi ya kufunga katika uwanja wa nyumbani
kwenye michuano ya Champions League msimu wakiwa wameshafunga mabao 13.
Barcelona
wamefanikiwa kufika nusu fainali ya ligi ya mabingwa ya ulaya mara sita
mfululizo, rekodi bora kabisa katika michuano hii.
Lionel
Messi (mabao 66) amebakiza mabao matano 5 tu kufikia rekodi ya mabao
Raul ya kufunga mabao mengi katika Champions League (mabao 71). Amefunga
mabao 7 katika mechi 4 msimu huu - akiwa kapiga mashuti 9 tu langoni.
Xavi
ameshaichezea Barcelona mechi 138 katika Champions League. Ikiwa
atacheza leo ataifikia rekodi ya kucheza mechi nyingi katika michuano
hii inayoshikiliwa na Ryan Giggs aliyecheza 139.
0 comments: