BAADA KIMYA CHA MUDA MREFU MISS TANZANIA HAPENESS WATIMANYWA AIBUKA NA KUNENA MZITO




Miss Tanzania 2013, Hapiness Watimanywa.
Miss Tanzania 2013, Hapiness Watimanywa, ameibuka na kusema kuwa kunyakuwa taji la urembo wa Miss Tanzania sio tiketi ya kuwa na skendo mbalimbali au kufanya mambo ambayo ni kinyume na maadili.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Happy alisema kuwa anaamini siyo kwamba mtu anapopata taji la urembo ndiyo linampa kichwa cha kuwa mcharuko, bali inategemea na uelewa wa mtu na mtu.

“Mimi sitaki kuamini kabisa kuwa unapokuwa mrembo ndipo tabia chafu zinaibuka bali ni malezi ambayo yanatofautiana miongoni mwetu,” alisema.
Mrembo huyo akaongeza kuwa, kwa upande wake anaamini atamaliza mwaka wake wa urembo akiwa ni msafi na wanaosubiria ang’are kwa skendo watasubiri sana.

0 comments:

Copyright © 2013. MSANGIBIN ALLY - All Rights Reserved
Customized by: MSANGIYUSUPHALY | Powered by: KIINICHAHABARI
Designed by: http://kiinichahabaribongo1.blogspot.com/