ASKARI FFU Z’BAR AUAWA KWA RISASI habari kamili hii hapa soma mwenyewe kujua
"Majambazi
walifanikiwa kumpora bunduki aina ya SMG na kisha kumpiga risasi na
kumjeruhi begani, tuko katika msako mkubwa hivi sasa,"Kamishna wa Polisi
Zanzibar.
Zanzibar.Askari
wa Kikosi cha FFU, Mohamed Mjombo (Namba E 5607) ameuawa kwa kupigwa
risas, huku mwingine akijeruhiwa baada ya majambazi kuvamia hoteli ya
kitalii ya Pongwe Bay iliyo Pongwe mkoani Kusini Unguja.
Akizungumza
na gazeti hili jana, Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame
alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 3:00 usiku wakati wageni wakiwa
wamepumzika na askari hao wa FFU kutoka Kituo cha Polisi Machui wakiwa
katika lindo kwenye hoteli hiyo.
Kamishna
Hamdan alisema muda huo lilifikagari moja na baada ya kuegeshwa watu
watatu waliteremka na kumvamia askari mweye Namba F 6198, Ibrahim Juma
Mohamed na kujaribu kumnyang'anya silaha aina ya SMG na katika
purukushani hiyo walimpiga risasi ya begani.
Alisema askari huyo anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Mnazi Mmoja.
"Majambazi
walifanikiwa kumpora bunduki aina ya SMG na kisha kumpiga risasi na
kumjeruhi begani. Tuko katika msako mkubwa hivi sasa," alisema Kamishna
huyo wa Polisi Zanzibar.
Hata
hivyo, alisema wakati Mjombo akisonga mbele kujaribu kumsaidia mwenzake,
alifyatua risasi lakini ikakwama katika chemba na majambazi hao
kufanikiwa kumpiga risasi sehemu ya ubavu na kutoroka.
Alisema
askari huyo wa FFU alifariki majira ya saa 7:00 usiku katika Hospitali
ya Mnazi Mmoja na kuzikwa jana huko Bambi Mkoa wa Kaskaszini Unguja.
Watu wawili wanashikiliwa na polisi kuhusiana na tukio hilo na wengine
wanaendelea kusakwa.
"Tayari
tumepeleka kikosi cha askari maalumu kutoka Mkoa wa Mjini Magharibi na
Mkoa wa Kusini Unguja, ili kuhakikisha usalama unaimarishwa katika
maeneo ya ukanda wa utalii," alieleza Kamishna Hamdan.
Daktari
bingwa wa Hospitali ya Mnazi Mmoja, Msafiri Marijani ambaye ndiye
aliyemfanyia uchunguzi Mjombo, alisema askari huyo alipoteza damu nyingi
baada ya kupigwa risasi ubavu wa kushoto na kutokeapaja la kulia na
ndio maana alipoteza maisha.
"Uti wa
mgongo pia ulivunjika," alisema Dk. Marijani. "Amepoteza damu nyingi
iliyokuwa ikivuja ndani ya tumbo na nje. Risasi bado haijapatikana
mahali ilipo mwilini."
Akizungumzia
tukio hilo, mwenyekiti wa Jumuiya ya Uwekezaji Katika Sekta ya Utalii
Zanzibar (ZAT), Abdulswamad Said alisema wakati umefika kwa SMZ
kuimarisha ulinzi katika Ukanda wa Utalii kwa vikosi vya SMZ na Polisi
kufanya kazi pamoja ili kulinda wawekezaji, watalii na wananchi.
Abdulswamad
alisema uongozi wa ZAT uliwahi kukutana na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali
Mohamed Shein na kuomba vikosi vya SMZ viongezewe nguvu za ulinzi ili
kukabiliana na matukio ya uhalifu na kusema jambo la kushangaza pamoja
na Rais kutoa agizo hilo, hakujawa na utekelezaji wa wazi.
"Matukio
ya watu kumwagiwa tindikali, milipuko ya mabomu na uhalifu wa kutumia
silaha hayatoi sura nzuri kwa maendeleo ya utalii Zanzibar. Juhudi zaidi
zinahitajika kukabiliana na vitendo hivyo hatari," alisema mwenyekiti
huyo wa ZAT.
Taarifa
kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa majambazi hao walikuwa wamebeba
silaha za kivita na kuaminika huenda walikuwa na silaha aina ya AK 47,
lakini hawakufanikiwa kupora mali hotelini hapo.
0 comments: