AJALI..PICHAZ..LORI LAIGONGA BODABODA DAR...TAZAMA PICHAZ HAPA...


Pikipiki 'bodaboda' ikiwa imekanyagwa na tairi la Scania.

Gari aina ya Scania likionekana kwa mbele likiwa limesimama baada ya ajali hiyo kutokea.

Bodaboda ikiwa nyang'anyang'a baada ya kukanyagwa na Scania.

AJALI  hii imetokea jioni ya leo eneo la Sinza-Palestina, Dar baada ya lori aina ya Scania lenye namba za usajili T303 ABV kuigonga pikipiki inayotumika kubeba abiria maarufu kwa jina la bodaboda.

Ajali hiyo iliwashangaza watu waliokuwepo karibu na eneo hilo kwani ilikuwa ni ya kushtukiza ambayo ilimwacha kila mtu mdomo wazi.

Hakuna mtu aliyejeruhiwa katika ajali hiyo japokuwa pikipiki iliharibika vibaya.

0 comments:

Copyright © 2013. MSANGIBIN ALLY - All Rights Reserved
Customized by: MSANGIYUSUPHALY | Powered by: KIINICHAHABARI
Designed by: http://kiinichahabaribongo1.blogspot.com/