AFRIKA KUSINI YAWATIMUA MABALOZI 3 WA UBALOZI WA RWANDA NCHINI HUMO....RWANDA NAYO YAJIBU MAPIGO KWA KUWATIMUA MAOFISA 6 WA UBALOZI WA AFRIKA KUSINI
SERIKALI ya Rwanda, imefukuza maofisa sita wa ubalozi wa Afrika Kusini muda mfupi baada ya nchi hiyo kuwataka maofisa watatu ubalozi wa Rwanda kuondoka Afrika Kusini.
Aidha,
kutokana na hatua hizo, Afrika Kusini imeanza kuangalia uwezekano wa
kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Rwanda, kutokana na mvutano wa siku
za hivi karibuni kati ya nchi hizo mbili, uliosababisha kila upande
kufukuza maofisa ubalozi.
Waziri
wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Louise Mushikiwabo amethibitisha Serikali
yake kuwafukuza maofisa sita wa Ubalozi wa Afrika Kusini, kwa madai kuwa
Serikali ya Afrika Kusini imewa hifadhi waasi waliojihusisha na
mashambulizi ya kigaidi.
“Tumewafukuza
wanadiplomasia sita wa Afrika Kusini kuwajibu na pia ni kutokana na
wasiwasi wetu kuwa nchi hiyo inawahifadhi waasi ambao wanahusika na
mashambulizi ya kigaidi nchini Rwanda,” alisema waziri huyo.
Afrika
Kusini ilichukua hatua hiyo ya kuwafukuza maofisa wa Rwanda, baada ya
nyumba ya mpinzani wa Rwanda, Jenerali Kayumba Nyamwasa anayeishi Afrika
Kusini kushambuliwa mapema wiki iliyopita jijini Johannesburg.
Gazeti
la Sunday Times nchini Afrika Kusini, lilinukuu chanzo cha habari
kutoka kitengo cha diplomasia, kikibainisha kuwa Afrika Kusini
wanaangalia uwezekano wa kumrudisha nyumbani Balozi wao aliyeko Kigali.
0 comments: