UNAFAHAMU HILI: Zabibu ni kinga dhidi ya Ugonjwa wa Moyo HABARI NZIMA HII HAPA
Hivi karibuni uchunguzi mpya umeonyesha kwamba kula zabibu au vyakula vyenye zabibu ndani yake kunapunguza shinikizo la damu, husaidia moyo kufanya kazi zake vyema na kupunguza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo uliotolewa kenye mkutano wa Majaribio ya Baiolojia huko California, zabibu zina uwezo wa kupunguza shinikio la damu, husaidia mwili uweze kuvumilia sukari (glucose tolorance) na kupunguza kiwango cha mafuta aina ya triglycerides mwilini ambayo ni chanzo cha matatizo ya moyo.
Wataalamu wanasema zabibu pia zinaweza kupunguza uvimbe, uharibifu unaotokana na free radicals zinazozalishwa mwilini na shinikizo la moyo.
Kwa ujumla zabibu zinazuia hali inayoitwa Metabolic Syndrome suala ambalo linatokana na mada za phytochemicals zilizoko kwenye matunda hayo.
Metabolic Syndrome ni mchanganyiko wa matatizo ya kitiba ambayo yanaongeza uwezekano wa kupatwa na maradhi ya mishipa ya damu pamoja na kisukari.
Hivyo wataalamu wanatushauri tule zabibu au kuongeza zabibu katika vyakula wanavyokula kila siku, ili tujikinge na ugonjwa wa Metabolic Syndrome, ugonjwa wa moyo na kisukari.
0 comments: