BENKI YA DUNIA YASITISHA MSAADA WA DOLA MILIONI 90 KWA UGANDA
Wakati
Facebook, WhatsApp na Instagram ikitishia kuondoa huduma zake nchini
Uganda baada ya Rais Yoweri Museveni kuidhinisha sheria mpya
inayoharamisha mapenzi ya jinsia moja, Benki ya dunia nayo imebana
msaada wa dola milioni 90 kwa nchi hiyo.
Benki
hiyo imesema kuwa inataka kufanya tathmini yake kuhakikisha kuwa
malengo yake ya maendeleo nchini Uganda katika sekta ya afya, ambayo
msaada huo ulikuwa unanuiwa, hayataathirika . Sheria iliyoidhinishwa na
Rais Yoweri Museveni, ilitiwa saini Jumatatu na inatoa adhabu kali kwa
watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
Wafadhili
wengine tayari wameanza kusitisha misaada Uganda. Wahisani kama Denmark
na Norway wamesema kuwa wataanza kufadhili mashirika moja kwa moja
badala ya serikali. Asilimia 20% ya bajeti ya Uganda inategemea michango
ya wafadhili.
Mpaka
sasa nchi tatu za Ulaya zimeamua kukata misaada yao kwa mamilioni ya
dola. Wizara ya fedha ya Uganda imesema inasubiri mawasiliano rasmi ya
nchi husika, na iko tayari kukabiliana na athari za hatua hiyo.
Hadi
kufikia sasa Waziri wa Fedha Wa Sweden, akiwa mjini Kampala, alisema
waekezaji kutoka nchi yake watakuwa na wakati mgumu kuweka pesa zao
nchini Uganda kwa sababu watakuwa na hofu kuwa sheria yo yote inaweza
kupitishwa kuwadhulumu watu.
Jana
serikali ya Uholanzi ilisema itazuia kwa muda misaada kwa Serikali ya
Uganda. Denmark pia zimetangaza kupunguza au kusimamisha kwa muda
misaada yake kwa Uganda.
0 comments: