UKIZINGATIA VIDOKEZO HIVI LAZIMA UWE NA MAISHA YA MAFANIKIO NA UTAJIRI...CHEKI HAPA
![]() |
Mwenyekiti Mtendaji Wa Makampuni Ya IPP Media Ltd, Dk. Reginald Mengi |
KILA mara
nimekuwa nikiwaeleza watu wangu wa karibu kuwa maisha yako ya baadaye
yanaanza na kile unachokifanya leo. Kama wewe unatamani maisha ya
kitajiri, basi msingi wake unakutegemea jinsi utakavyoanza kuujenga hivi
sasa.
Wapo baadhi
ya watu wana ndoto za maisha mazuri na ya kitajiri kwa kutegemea yaje
kama wanavyoota. Wengine utawasikia ipo siku watakutana na wanawake au
wanaume wenye fedha, ambao watawapa maisha wanayohitaji kirahisi.
Kuishi kwa
matumaini hayo ni kupoteza muda, lakini amini nikuambiayo, unaweza
kuishi maisha unayoyataka kama utaanza kujiandaa kuanzia hivi sasa,
kwani hata umaskini walionao wananchi wengi, ni wa kujitakia, ingawa
baadhi yao, miundombinu duni ya nchi yetu imechangia.
Hapa chini,
nimekuwekea baadhi ya vidokezo kadhaa, ambavyo kama utavizingatia,
vinaweza kukusaidia kukupatia maisha yenye mafanikio na hivyo kutimiza
ndoto zako za muda mrefu.
Kinachobakia katika matumizi yako ni mtaji
Watu wengi wamekuwa hawajui kuwa kila senti inayobaki baada ya matumizi yako basi ni mtaji mkubwa wa kukusaidia kufikia malengo. Staili ya maisha ya wengi yanawafanya wajiandae kuwa maskini au watu wa daraja la kati badala ya utajiri.

Kuna watu
wana maisha mazuri kiasi kwamba wanajimudu kutengeneza bajeti zao za
vyakula na matumizi muhimu kwa mwezi mzima kwa fedha za mishahara yao au
biashara wanazofanya.
Baada ya bajeti ya vitu muhimu kukamilika na kutekelezwa, kinachobakia huwa ni matumizi mengineyo kwa fedha zote zilizobakia kwenye mishahara yao.
Baada ya bajeti ya vitu muhimu kukamilika na kutekelezwa, kinachobakia huwa ni matumizi mengineyo kwa fedha zote zilizobakia kwenye mishahara yao.
Wapo pia
ambao akiba yao huitunza benki au hununulia vitu vya bei kubwa kama
vitanda, makabati, televisheni, magari na kadhalika.
Katika
hesabu za kuelekea kwenye mafanikio, unahimizwa kutopenda sana kuweka
hela ‘iliyokufa’. Hela hii ni ile unayohifadhi benki au kununulia vitu
ambavyo haviwezi kukupa faida.
Watu wa uchumi na wajasiriamali waliofanikiwa, wanakushauri kuwa akiba unayopata kuwekeza katika kupata vyanzo vipya vya mapato yako.
Mipango yako ya matumizi ni dhahabu
Wote tunajua kwamba dhahabu ni jiwe lenye thamani ambalo kila mmoja angetamani kulipata, hasa likiwa ni kubwa. Mipango yetu ya matumizi ni sawa na madini haya yenye thamani. Ukitaka kujua uimara wa mtu kifedha, angalia jinsi mipango yake ya matumizi ilivyo.
Chukulia mipango ya watu wawili tofauti ifuatayo

Mtu wa kwanza: Anachangia kwa wasiojiweza. Anajiwekea akiba. Ananunua vitabu vya uwekezaji. Semina ya mashamba. Muda wa mazoezi.
Mtu wa pili: Bia sita kila siku.
Ananunua viatu vipya.
Mtu wa pili: Bia sita kila siku.
Ananunua viatu vipya.
Nunua TV mpya. Tiketi za soka. Bia zingine sita.
Mfano huu mdogo unakuonyesha aina mbili tofauti kabisa ya watu. Mmoja hafikirii kabisa kuhusu kesho yake. Unachogundua ni kwamba wakati mmoja anawekeza na kujiandalia kuhusu kesho, fedha za mwingine zinaonyesha zinatoka tu mfukoni zikiwa hazina mrejesho.

Ili kujua
kama unaandaa kesho yako iliyo nzuri, angalia mipango yako ya matumizi
ya fedha, ndipo utakapojua jinsi unavyoipa thamani dhahabu uliyoishika
au unavyoifuja bila wewe mwenyewe kujua.
Tumia ulichonacho kwa ukomo
Tumia ulichonacho kwa ukomo
Kila siku,
watu wanaotafuta mafanikio katika maisha yao hawaishi na wala
hawaridhiki na walipo. Wanaamini katika kuwekeza, kwa kuwa kutawawezesha
kutimiza kila ndoto waliyonayo.
Lakini lipo tatizo la baadhi ya watu kuanza kuridhika na mafanikio madogo yanayojitokeza mbele yao. Badala ya kuendelea kuwekeza, tena na tena, wao huanza kutapanya mali zao kana kwamba wanazo nyingi kiasi hazitakwisha.

Huku ni
kujidanganya. Mtu anayesaka mafanikio, hata kama atatamani kununua kitu
kizuri, hatauza mali aliyonayo ili anunue, bali atatafuta mbinu zaidi za
kufanya ili apate anachokitaka.
Atatafuta
vyanzo zaidi vya mapato ambavyo kwa vyovyote, vitaongeza kiasi cha fedha
anachoingiza kila mwezi na kwa maana hiyo, baada ya muda atajikuta
amepata kile alichokitaka bila kupoteza mali yoyote aliyokuwa nayo
kabla. Hivyo ndivyo walivyofanya akina mzee Reginald Mengi, Rostam
Azizi, mzee Saidi Bakhresa na wengine wengi waliotajirika.
0 comments: