KESI YA SHEIKHE PONDA YAAHIRISHWA HADI MEI 14 , MWAKA HUU
Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mkoa
wa Morogoro kwa mara nyingine leo imeshindwa kuanza kusikiliza kesi ya
Katibu wa Taasisi na Jumuiya ya Waislamu Tanzania , Shehe Ponda Issa
Ponda kutokana na jadala halisi kutorejeshwa kwenye Mahakama hiyo
toka Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam na hivyo
kuiahirisha hadi Mei 14, mwaka huu.
Katibu wa Taasisi na Jumuiya ya Waislamu Tanzania , Sheikhe Ponda Issa Ponda ( mwenye kanzu) akiwa ndani ya chumba cha Mahakama akisubiri hatima ya kesi yake |
Katibu wa Taasisi na Jumuiya ya Waislamu Tanzania , Sheikhe Ponda Issa Ponda ( mwenye kanzu) akisindikizwa na baadhi ya Askari Kanzu na wakawaida , kutoka Mahakamani |
Baadhi ya wafuasi wa Katibu wa Taasisi na Jumuiya ya Waislamu Tanzania , Sheikhe Ponda Issa Ponda wakitoka kwenye viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro |
Shehe
Ponda alifikishwa Mahakamani hapa majira ya saa tatu asubuhi chini ya
Ulinzi mkali wa Polisi ,ambapo pia baadhi ya wafuasi wake walifika
mapema Mahakamani hapo wakitakiwa kubakia nje ya uzio .
Hakimu
Mkazi Mwandamizi wa Mkoa , Mary Moyo , anayesikiliza kesi hiyo alitumia
dakika tatu kufikia kutoa maamuzi kuahirisha kutokana na Jadala
halisi la kesi kuendelea kubakia Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Aliufahamisha
upande wa wakili wa serikali na Wautetezi kuwa hakuwa na jalada halisi
la kesi hiyo na bado haijarejeshewa toka Mahakama Kuu Kanda ya Dar
es Salaam, lilipopelekwa kwa ajili ya kusikilizwa ombi la Sheikhe
Ponda la mapitio lililowasilishwa kwenye Mahakama kuu hiyo siku za
nyuma.
Sheikhe
Ponda amefuguliwa kesi namba 128/2013 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
mkoa wa Morogoro akikabiliwa na Mashitaka matatu ambayo aliyatenda
Augosti 10, 2013, eneo la Kiwanja cha Ndege, Manispaa ya Morogoro na
alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Augosti 19, 2013.
Source:Mdau John nditi
0 comments: