KUPATA AJIRA NJE YA TANZANIA KUPO HIVI.....Soma zaidi hapa
1. Kazi zenye mahitaji maalum :
Hizi
ni kazi
za fani mbalimbali ambazo serikali za nchi kadhaa hutangaza kuwa nchi
husika
inahitaji sana watu wa fani husika. Serikali ya nchi husika hutoa
muongozo wa jinsi mashirika/asasi mbalimbali zinavyoweza wasilisha
maombi ya mahitaji maalum ya kuajiri.Mfano nchi kama Afrika Kusini mwaka
2011 ilitoa muongozo ufuatao. Bofya hapa kusoma.
La msingi kukumbuka hapa ni kuwa uhitaji maalum huu sio kwamba
serikali ndio inahitaji kuajiri watu hapana, ni taifa kwa ujumla- serikali,
mashirika na makampuni mbalimbali ya nchi husika yanahitaji kuajiri watu wa
hizo fani zenye mahitaji maalum. Kwa
msingi huu,michakato na taratibu za uhamiaji –kutoa vibali vya kazi, huwa si
ngumu sana kama ilivyo katika aina nyingine za kazi.
2. Kazi zenye ushindani:
Hizi ni kazi ambazo
si lazima ziwe zimetangazwa kuwa za mahitaji maalum kwa taifa, hata hivyo
mashirika na makampuni ya nchi husika hushindana katika kupata watu bora wa
kufanya kazi husika. Mfano wa kazi hizo ni graphics designers,
3. Kazi za kawaida: Hizi ni aina nyingine ya kazi ambazo haziingii katika
makundi yaliyotajwa hapo juu. Mfano kazi za mikataba ya muda mfupi,
kubadilishana wafanyakazi –mfano mtanzania kuhamia Kenya na Mkenya kuhamishiwa
Tanzania. Kundi hili pia linajumuisha ajira kwa wanamichezo na wasanii.
Jinsi ya kupata taarifa za ajira za nje ya
Tanzania
Unaweza
kupata taarifa za nafasi za kazi zilizopo huko nje ya Tanzania kwa kupitia njia
mbalimbali kama vile:-
1.Marafiki/Ndugu
na jamaa waishio nje ya Tanzania:
Kwa kutumia marafiki , ndugu , na jamaa ambao
wana taarifa sahihi na zinazoweza kukusaidia kuhusu soko la ajira, unaweza
kujikuta unapata taarifa muhimu. Nafasi
nyingi zinaweza kuwa zinapatikana ila hazitangazwi kwenye vyombo vya habari ,
hivyo marafiki, ndugu , na jamaa waishio huko nje ya Tanzania, wanaweza
kukudokeza ‘michongo’ iliyopo na jinsi unavyoweza kuifanyia kazi. Ni muhimu
kudadisi vema ili ujue aina ya kazi, sifa zinazohitajika , malipo na mazingira
ya kazi kabla haujafanya maamuzi ya kusafiri kwenda kuapply au kufanya
interview.
2.. Mitandao ya kijamii:
Ukitembelea baadhi ya pages za mashirika na makampuni hutangaza nafasi za kazi kwa kurasa zao za mitandao ya kijamii. Mfano mzuri ni Microsoft Africa kama unavyoweza jionea tangazo hili hapa chini kwenye picha, toka kurasa yao ya Facebook:
3. Website za Makampuni na Mashirika:
Tembelea websites na hata blogs za mashirika
na makampuni mbalimbali yaliyopo nje ya Tanzania, na tazama kama wameweka
tangazo/matangazo ya nafasi za kazi.
4. Website za mawakala wa ajira (Recruitment
Agents):
Kuna mashirika au makampuni
maalum yanayojishughulika na kuajiri kimataifa. Mawakala hawa hutangaza nafasi
za ajira na pia hutoa maelezo ya mchakato wanaotumia kufanikisha mtu kupata
ajira. Hata hivyo kuwa makini na mawakala hewa wanaotanguliza kudai malipo.
Baadhi ya Mawakala wa ajira na websites zao ni kama ifuatavyo:
5.Websites za watangazaji wa ajira:
Kuna websites kadhaa zenye kujishughulisha na kuweka hewani matangazo ya ajira kutoka mashirika, makampuni mbalimbali na mawakala wa ajira. Unaweza ku search kwa kutumia Google kwa kuandika neno mfano Accounting jobs in Sudan, na kupata maelezo majibu ya Google yakiorodhesha websites za watangazaji wa ajira au websites za mashirika/makampuni husika. Pia waweza tembelea websites za watangazaji wa ajira maarufu kama vile:
6. Linkedin:
Mtandao maalum kwa watu wa
fani mbalimbali, ambapo pia makampuni na mashirika mbalimbali hutangaza nafasi
za ajira. Pia waweza chagua huduma ya Linkedin ambapo utakuwa ukitumiwa taarifa
za nafasi za kazi kwa kadri ya uzoefu na ujuzi wako uliorodhesha katika wasifu
wako, na pengine kwa uchaguzi wa aina ya nafasi za ajira unazotaka kufahamu.
Usisubiri mpaka utumiwe matangazo, waweza tembelea kurasa husika za mashirika
na makampuni humo Linkedin na kutambua nafasi za ajira zinazotangazwa.
Taarifa kutoka kampuni au shirika ulilopo sasa: Pengine kampuni au shirika ulilopo lina utaratibu wa kubadilisha maeneo ya kazi ya wafanyakazi wake. Fuatilia kujua mchakato mzima wa kubadilishwa eneo la kazi upoje, masharti na lini mabadiliko (transfer) hayo hufanyika. Hii inaweza kuwa nafasi yako ya kujiandaa kuhamishiwa nje ya Tanzania kwani waweza kutambua vigezo ya kiutendaji au kielimu unavyotakiwa kuwa navyo ili upewe ‘promotion’ ya kuenda nje ya Tanzania.
Masharti ya kufanyakazi nje ya Tanzania
1. Uhakiki
wa vyeti vyako:
Baadhi ya nchi za nje
hutaka kuwa waombaji wote wa vibali vya kazi wahakiki vyeti vyao kupitia
mamlaka au taasisi maalum ya nchi hizo ili kujiridhisha kuwa kweli vyeti vyako
ni halali, na kwamba aina ya kiwango cha elimu ulichonacho kinaendana na
viwango vya elimu vya nchi hizo.
2. Kuandikishwa
katika mamlaka au wakala fulani wa fani husika:
Baadhi ya nchi za nje hutaka kuwa waombaji wote wa vibali vya kazi wawe
wamehakikiwa na kuandikishwa na mamlaka zinazohusika na fani ambayo muombaji wa
kibali cha kazi anataka . Mfano kama ni mhasibu basi awe ameandikishwa na bodi
ya wahasibu ya nchi husika.
3. Kuwa na Passport:
Ni lazima uwe na
passport halali na pia isiwe imeisha muda wake, na kwamba wakati wa kuomba
kibali cha kazi , ni lazima uwe na viza isiyoisha,yaani bado una uhalali wa
kuishi nchi husika walau kwa mwezi mmoja zaidi kama unafanya maombi ya kibali
cha kazi ukiwa katika nchi husika huko ughaibuni.
4. Malipo ya kibali cha kazi:
Malipo ya
kibali cha kazi, hutofautiana kati ya nchi na nchi.
5.Taarifa ya polisi:
Hii
ni taarifa ambayo polisi nchini Tanzania wataitoa kueleza kuwa wewe si
mhalifu au mhalifu. Kabla ya polisi kutoa taarifa hii hufanya uchunguzi
wa maabara wa alama zako za vidole.
Mambo Mengine ya msingi kuzingatia
1. Lugha:
Lugha ndio kiungo cha mawasiliano,
kwahiyo ni muhimu kutambua lugha kuu ya mawasiliano ya eneo husika, na
kujitahidi kuweza kuzungumza kwa ufasaha na pia ujiandae kujifunza lugha ndogo
za mawasiliano ya kila siku. Mfano mzuri wengi hujidanganya na ‘Kiswanglish’
yaani kule kuzungumza kiswahili kisha ukachomekea na maneno machache ya
kiingereza basi ndio ukajiona unaifahamu lugha. Jitahidi uiweze vema lugha
husika kwani huko uendako hautopata muda wa kuchanganya kiswahili na lugha ya
kigeni. Hata hivyo ni jambo la kukumbuka
ukiwa makini na kwa jitihada za uhakika, utaweza kujikuta unaifahamu vema lugha
ngeni kwa haraka.
2.Utofauti wa tamaduni:
Kuna tofauti
nyingi za jinsi watu wanavyoishi katika nchi nyingine , mfano aina ya vyakula
wanavyokula, mavazi, jinsi
wanavyoheshimiana, kusalimiana, kuabudu, aina za nyumba, usafiri, n.k Uwe tayari
kukabiliana na utofauti huo wa tamaduni na ujifunze kuheshimu tamaduni za
wengine.
3. Gharama za maisha:
Inapendeza zaidi
ukifanya utafiti wa gharama za maisha za nchi husika unayotarajia kuishi ili
kujua jinsi kipato chako kitakavyotumika na jinsi utakavyoweza kuweka akiba kwa
ajili ya shughuli nyinginezo za ndoto zako. Nchi nyingi zilizoendelea zina
gharama kubwa za maisha hivyo kujikuta unaishia kutumia sehemu kubwa ya mapato
yako kwa kula na kujikimu tuu.
4. Ajira ni bidhaa:
Mtu,shirika au kampuni, hutangaza nafasi ya
kazi ili kuweza kupata mtu atakayefanyika shughuli fulani kwao. Hivyo kuendana
na ujuzi wako na uzoefu wako, unajikuta unatakiwa uwahakikishie au uwaridhishe
hao waajiri kuwa kweli utaweza kufanya hayo wanayotaraji wewe kufanya. Hii ni
kama kuuza bidhaa, ambapo ni lazima kumfanya mteja aone sababu ya kununua
bidhaa yako. Andaa vema wasifu wako (CV/RESUME), andika kwa ufasaha barua ya
maombi ya kazi ukijieleza vema kwa kulinganisha maelezo ya nafasi husika
unayoomba, uzoefu wako na ujuzi wako.
Usikate tamaa pale maombi yanapokosa majibu, endelea kuaply sehemu nyingine.
5. Utayari wa kuishi
katika nchi husika:
Inapendeza pia ukapata taarifa za awali kuhusu nchi
husika unayofikiria kufanya kazi. Tumia mitandao ya kijamii, websites na hata
mawasiliano ya moja kwa moja ya watu waishio huko ili kujua hali ya hewa,
tamaduni, gharama za maisha na mambo mengine unayoona yanaweza kuathiri maisha
yako. Pia ukiwa na nafasi wewe mwenyewe funga safari uende kuitembelea nchi
husika ukae walau mwezi mmoja au wiki kadhaa hivi, ili kujifunza zaidi kuhusu
nchi husika na kujipima kama kweli upo tayari kuishi nchi husika.
0 comments: