HAYA MAZITOO SANAA..... WANAUME NAOMBA USHAURI WENU -MUME WANGU SIMUELEWI


Mimi ni mama wa mtoto mmoja wa miaka 5 na nina mume wangu wa ndoa zaidi ya miaka sita. ila mume wangu simwelewi kitu kimoja inafika kipindi akaninunia na asikwambie sababu na ukimuuliza nini mbaya unaweeza ukalamba
hata vibao. si mara moja ili swala kujitokeza ndo mana nimeona nilete jamvini. na anakuwa na majibu ya mkato na hasira endapo nitamuuliza kitu. yani nakuwa sina thamani kwake. na naweza nikawa nyumbani na apigi kwa simu yangu anapiga ya dada na anaweza sa nyingine akarudi usiku wa manane na yupo chakali. sasa na jiuliza uu ni ugonjwa ama pepo. akiwa ajaninunia yupp sawa na ni mume mwema. ila haiwezi pita miezi 3 ajaninunia.

je mnahisi ana tatizo gani? mi nampenda sana mume wangu. ila kama binadamu akiwaga na khali hiyo nami uwa naumia mpaka sa nyingine nawaza yasiyo wazika.

0 comments:

Copyright © 2013. MSANGIBIN ALLY - All Rights Reserved
Customized by: MSANGIYUSUPHALY | Powered by: KIINICHAHABARI
Designed by: http://kiinichahabaribongo1.blogspot.com/